KAMPUNI ya Azam Media Limited, leo imetangaza kuwa Tido Mhando ameteuliwa kuwa kaimu-Mkurugenzi mtendaji, Uhai Production Ltd.(UPL). Tido, anaungana na Rhys Torrington ambaye ni Mkuregenzi Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd na mtangazaji huyo maarufu wa mpira zamani nchini, Mhando ataanza majukumu yake mara moja, ikiwa jukumu lake kubwa ni utengenezaji na uboreshaji wa vipindi vya kitanzania katika televisheni na redioni.
Mhando mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40 kwenye tasnia ya utangazaji na
Uandishi wa Habari, ni mtu anayejulikana na kuheshimika katika tasnia
hiyo ukanda wa Afrika Mashariki na Ulimwenguni kote.
Tido Mhando sasa wa Azam TV |
Alianza kazi kama DJ Radio
Tanzania na mnamo mwaka 1985 alijiunga na BBC idha ya Kiswahili Nairobi
kama mwandishi wa habari. Ukuwaji wake ndani ya shirika ulimpelekea
kuhamishiwa jijini London mwaka 1991 ambapo aliteuliwa kuwa Mwafrika wa
kwanza kuongoza idara ya Idhaa ya Kiswahili BBC.
Baada
ya kurejea Tanzania, Mhando ameshika nyadhifa mbali mbali za juu
zikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TBC na hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa
Mwananchi Communication Ltd.
Akizungumzia
uteuzi wake, Mhando amesema; “Ninayo furaha kubwa kujiunga na Azam
Media, pia na changamoto kubwa zilizopo mbele yetu kuifanya kuwa kampuni
pekee ya Televisioni na Redio yenye ubora katika kutoa burudani hapa
nchini (Tanzania) pia na ukanda wote wa Afrika,”.
Mhando ofisi zake zitakuwepo katika jengo la kisasa la Uhai Production
Tabata, Dar es salaam. UPL inajulikana kwa ubora wake katika kurusha
matangazo yake moja kwa moja kama vile, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara pamoja na vipindi vingine maarufu kama Kwetu House na Morning
Trumpet.
Pia katika wiki zijazo UPL itazindua studio zake mpya zenye kiwango cha
kimataifa ambazo zitamuwezesha Mhando kuwa na uwezo mkubwa wa
kutengeneza vipindi mbali mbali vyenye viwango vya kimataifa
akishirikiana na watengenezaji wazawa.
Akizungumzia
uteuzi huo, Muingereza Torrington amesema: “Tunayo faraja kubwa kwa
Tido kujiunga nasi wakati tunakaribia kutimiza mwaka wetu wa kwanza
tokea tuanze kutoa huduma, inanipa furaha kwamba Azam TV imekuwa kwa
kasi na kuwa wasambazaji wakuu na watoa huduma bora satellite Pay Tv
Tanzania,”.
“Kwa
uzoefu wake nategemea Tido atachukuwa jukumu la kutupeleka katika hatua
nyingine ya mafanikio kibiashara kwa kutengeneza vipindi na burudani
mbali mbali kwajili ya wateja wetu Tanzania na kuvuka mipaka yetu. Na
mtakia kilala kheri katika majukumu yake mapya,” amesema.
No comments:
Post a Comment