1:-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, Mkuu wa mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, kwa pamoja
wakisimama kupokea maandamano wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku
ya Ukimwi Duniani iliyofanyika Desemba 1, 2014 Kitaifa kwenye Uwanja
wa Sabasaba Mkoani Njombe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani
zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe,
Desemba 1 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wakati akiondoka katika uwanja wa
Sabasaba baada ya kuhutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya
Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa huo Mkoani Njombe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipunga mkono kuwaaga wananchi wakati akiondoka uwanjani hapo baada ya
kuhutubia katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani,
zilizofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, akijumuika na wasanii wa Kikundi
cha Sanaa cha Kanisa la KKKT, wakati wakitoa burudani yenye ujumbe
kuhusu maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi Duniani.
Baadhi
ya wandamani wakipita mbele ya jukwaa kuu na mabango yenye ujumbe
mbalimbali kuhusu siku ya Ukimwi Duniani wakati wa sherehe hizo
zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe Desemba 1, 2014. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment