Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,
Rosalynn Mworia(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo
pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA
itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kufanya malipo ya huduma katika
sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki
huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari,Wengine katika picha
maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari kushoto ni Manase Banduka
Mkurugenzi wa Uendeshaji,kulia Mkurugenzi Mtendaji Andrew Mboma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa tovuti ya Vinjari Andrew Mboma(kulia)akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya
Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kufanya
malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa
njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari,
Wengine katika picha Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma
wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(katikati) kushoto ni Manase Banduka
Mkurugenzi wa Uendeshaji.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,
Rosalynn Mworia(kushoto)akipongezana na maafisa waandamizi wa tovuti ya
vinjari (katikati ) Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji,(kulia
)Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti hiyo Andrew Mboma wakati wa uzinduzi wa
huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom
kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na
utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti
hiyo.
Katika
kuzidi kurahisisha huduma za malipo wakati tukielekea msimu wa sikukuu
za Krismas na Mwaka Mpya,kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo
imezindua huduma mpya ya kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki.
Huduma
hii mpya inayozinduliwa leo inajulikana kama Vinjari na M-Pesa ambayo
itawawezesha wateja wa Vodacom kufanya malipo ya huduma katika sekta ya
usafiri wa ndege na utalii kwa njia ya kieletroniki kama ambavyo
yamekuwa yakifanyika kwa kutumia kadi mbalimbali za kufanyia malipo
kimataifa.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hii Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema huduma hii
kwa kuanzia itafanyika kwa kushirikiana na mtandao wa malipo ya
kieletronikali nchini ujulikanao kama Vinjari.co.tz ambao
unafanya kazi na zaidi ya taasisi 300 za kutoa huduma yakiwemo
mahoteli ya utalii na makampuni mbalimbali yanayotoa huduma hususani za
masuala ya utalii na sehemu za mapumziko na burudani.
“Kadri
siku zinavyozidi kusonga mbele tunazidi kushuhudia mapinduzi makubwa ya
kiteknolojia hususani katika masuala ya biashara, Vodacom tumeona
umuhimu wa kuanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wetu kufanya
miamala yao kwa njia ya kieletroniki kupitia huduma ya M-Pesa ili kwenda
na wakati zaidi. Kwa kuanzia tutatoa huduma hii kupitia mtandao mpana
wa malipo ya kielektronoki wa vinjari.co.tz na kadri siku zitakavyosonga mbele tutazidi kuboresha huduma hii,” alisema.
Aliongeza
kuwa Vodacom inaelewa kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawana kadi za
kimataifa za kufanya miamala ya malipo kwa njia ya kielekroniki ndio
maana imekuja na huduma hii ikiwa inawalenga wateja wetu wanaotumia
huduma ya M-Pesa.
Naye
Mkurugenzi wa Vinjari.com,Andrew Mboma amesema ili kupata huduma hii
mteja anaingia katika sehemu ya kawaida ya kufanya miamala ya M-Pesa
kwenye simu yake atakuta sehemu inayomuelekeza jinsi ya kupata huduma
kupitia Vinjari na M-Pesa ambapo ataweza kufanya muamala kwa kadri ya
huduma atakayokuwa anahitaji na atakatwa fedha kutoka akaunti yake ya
M-Pesa kulipia huduma hiyo na malipo kidogo ya kutumia huduma hiyo.
Maelezo zaidi yanapatikana kwa kutembelea tovuti ya vinjari.co.tz
Katika
miaka ya karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za
mkononi nchini ambapo pia kumekuwemo na ongezeko la watumiaji wa mtandao
wa internet.
Inakadiriwa
kuwa zaidi ya watanzania milioni 28 wanatumia huduma za simu za mkononi
ambapo zaidi ya watanzania milioni 6 wanatumia huduma za internet.
No comments:
Post a Comment