Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la
Neawala Mh George Mkuchika mara baada ya kuwasili mjini Newala akiwa
katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mtwara ziara yenye lengo la
kukagua na kuhimiza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010 inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu
Mkuu Kinana emeembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa
miondombinu ya maji , Zahanati Ofisi za Chama cha Mapinduzi na
kuzungumza na wananchi katika mikutano mbalimbali, Katika ziara hiyo
Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE -NEWALA-MTWARA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana
viongozi wa kiwanda cha kubangua korosho mjini Newala kulia Niry Patel
Mratibu wa Usafirishaji na katikati ni Ednyadayu Meneja wa ufundi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubangua korosho na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi ya kubangua korosho
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mhandisi wa Maji Newala Bw. Nsajigwa Said wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Malatu mjini Neawala.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa maji katika kata ya Malatu kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mtwara B. Halima Dendegu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kusuka nondo katika ujenzi wa tanki la maji la kijiji cha Kilidu kwa
pamoja na wafanyakazi wa katika mradi huo wa tatu kutoka kulia
aliyesimama ni Mbunge wa jimbo la Neawala Mh. George Mkuchika.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata
maelezo kutoka kwa Dr Yudas Ndugile Mganga mkuu wa wilaya ya Newala
wakati alipokagua jengo jipya la Kituo cha Afya Mkwedu kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa wilaya ya Newala BwMarx Simon Kamaoni na Mkuu wa mkoa wa
Mtwara Bi. Halima Dendegu.
Katibu
wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishuhudia aliyekuwa
Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda Sijaona
akivua shati la CHADEMA na kuvaa la CCM mara baada ya kuondoka katika
chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala.
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitupa shati hilo
Aliyekuwa
Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Newala Chadema Bw. Adam Nangwanda akiwa
amekabidhi kadi yake na ya mke wake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana mara baada ya kujiunga na CCM mjini Newala kulia ni
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiwahutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama mjini Newala
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakisisitiza jambo katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakikabidhi pikipiki kwa vijana ambazo zimekopeshwa kwao ili kujikomboa kiuchumi.
Umati wa watu wakisikiliza mkutano huo.
No comments:
Post a Comment