Mratibu wa shughuli za
ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Bw. Senya Tuni (Wapili kulia) akieleza jambo
mara walipoingia kwenye eneo la gati la Bandari ya Mbaba Bay. Wanaomsikiliza ni
Mkuu wa msafara huo, Bibi Florence Mwanri (Kulia), Afisa mazingira wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bw. Julius Edward (Watatu kulia). Na kushoto ni Bw.
Jordan Matonya ambae ni Mchumi kutoka Tume ya Mipango.
Na
Saidi Mkabakuli, Mbaba Bay
Timu
wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango imetembelea
Bandari ya kimkakati ya Mbaba Bay iliyopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bandari hiyo.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba Bandari
hiyo ni muhimu kwa uchumi wa nchi kwa kuzingatia eneo la kijiografia la bandari
hiyo.
“Bandari
hii ni muhimu kwani kijiografia inaweza kuzifikia nchini nyingi zilizo kusini
mwa nchi yetu hivyo inaweza kutumika kama lango la kibiashara miongoni mwa
jirani zetu licha ya uhaba wa miundombinu yake,” alisema.
Aliwasihi
wafanyakazi wanaoihudumia Bandari hiyo kufanya kazi kwa bidii bila ya kuchoka
ili kuweza kuvutia wafanyabiashara na watumiaji wengine kuendelea kuitumia
bandari hiyo.
Kwa
upande wake, afisa bandari ya Mbaba Bay, Bw. Jarome Urio aliutaarifu ugeni huo
kuwa Mamlaka ya Bandari ipo katika mkakati wa kuindeleza bandari hiyo ili
kuweza kuihudumia wateja wengi zaidi.
Pia,
Bw. Urio aliwashukuru wajumbe wa timu hiyo ya ukaguzi kwa kwenda kuitembelea na
kujionea maendeleo ya bandari hiyo.
“Tunafarijika
sana kuona viongozi wa serikali wanapokuja kututembelea kwani hali hii uongeza
hamasa ya utendaji kazi wetu,” alisema.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016) bandari
ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili
kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.
Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija
katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na
ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda:
Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda
vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo,
mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini
kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali.
Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya
rasilimali watu na ujuzi:
Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya
ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma) katika
kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na Utalii, Biashara,
na huduma za Fedha ambapo jitihada zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa
kuuza katika masoko ya ndani na nje, kuongeza
idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na kuongeza upatikanaji
wa huduma za kifedha.
No comments:
Post a Comment