Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Reginard Mengi, wakati
alipowasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Novemba 5,
2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji
Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji
Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF,
lililofanyika Novemba 5, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza
Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya ufunzi huo
uliofanyika Novemba 5, 2014, kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada
ya ufunguzi. Picha na OMR.
No comments:
Post a Comment