Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)
akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa kwanza wa Qatar nchini Tanzania
Mhe. Jassim M. Al-Darwish alipokwenda kumuaga rasmi baada ya kumaliza
muda wake wa kazi hapa nchini.
Waziri
Membe akizungumza jambo na Balozi Jassim M. Al-Darwish huku Mkurugenzi
wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (kushoto) akisikiliza.
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Batholomeo Jungu akisikiliza mazungumzo kati ya Waziri Membe na Balozi Al- Darwish ambao hawapo pichani
--------------Hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akitoa
neno la shukrani kwa Balozi wa Quatar Mhe. Jassim M. Al-Darwish, kwenye
Hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
kwa ajili ya kumuaga Balozi Al-Darwish ambaye amemaliza muda wake wa
kazi hapa nchini.
Sehemu ya
Wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
Ubalozi wa Qatar wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga pamoja na wageni wengine
waalikwa wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Membe (hayupo
pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish wa Qatar ambaye
amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Balozi
Jassim M. Al-Darwish akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kumuaga
ambapo alitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano aliopata
katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na kuomba ushirikiano huo
uendelee.
Sehemu ya
Wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Qatar akiwemo
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya (wa pili
kulia) wakimsikiliza Balozi huyo (hayupo pichani) alipowahutubia.
Waziri
Membe (Mb.) akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa Tembo Balozi
wa Kwanza wa Quatar nchini Tanzania Mhe. Al-Darwish wakati wa hafla
fupi ya kumuaga Balozi huyo ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa
nchini.
Picha ya Pamoja. Picha na Reginald Philip |
No comments:
Post a Comment