Inspekta
Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya
makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama
barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo
mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
Miongoni
mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa
kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit
Nsimeki anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa
kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa
anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.
Wengine
ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP)
Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa
Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda
amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa
kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma
amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Zaidi
ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi
Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga
anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa
upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David
Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma
Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora .
Aidha,
aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi
(SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa
Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela
anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa
upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi
anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
Kwa
upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na
aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum
Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa
Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni,
na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC
Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.
Wengine
ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James
Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu
wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe Buzema anakwenda
kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa
wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda
kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa
wa Njombe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda
kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.
Mabadiliko
hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi
la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma
bora ya usalama.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi
No comments:
Post a Comment