Waziri
wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika jijini Dar es
salaam” na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi
chini ya kauli mbiu isemayo “ Takwimu Huria kwa uwajibikaji na
ushirikishwaji wa wadau wote.
Mkurugenzi
wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda
Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu
matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo nchini
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika jijini
Dar es salaam.
Mtakwimu
Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza
jambo kuhusu athari, madhara na ya matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
Baadhi
ya wadau mbalimbali na wataalam wa takwimu waliohudhuria maadhimisho ya
Siku ya Takwimu Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali jijini Dar
es salaam.
Mwakilishi
kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto)
akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu
sahihi katika maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika jijini Dar es salaam.
Msanii
Stara Thomas (kulia) akiwa na waimbaji wenzake akiwasilisha ujumbe wa
matumizi ya takwimu sahihi kupitia wimbo maalum wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Takwimu Afrika yaliyowashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani
na nje ya nchi chini.
Waziri
wa Ferdha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee (wa nne
kutoka kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji na
watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, jijini Dar es salaam.Picha na
Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment