
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Abubakar Rajabu (aliesimama) akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wabunge
wa Kamati ya Huduma za Jamii,waliofanya ziara ya kutembelea na
kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo
ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na
Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo
Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katika ziara hiyo ya Wabunge chini ya
Mwenyekiti wao,Mh. Said Mtanda (katikati) walivutiwa sana na maendeoe ya
miradi hiyo na hivyo kulipongeza Shirika la NSSF kwa kazi nzuri
wanayoendelea kufanya.

Waziri
wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanya jambo
mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya
kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa
na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni
Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco
Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam

Mbunge
jimbo la Lindi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za
Jamii,Mh. Salum Barhan akifatilia kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja
la Kigamboni iliyokuwa ikitolewa na Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (hayupo pichani)

Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Manyovu Mkoani Kigoma,Mh. Albert Obama akiuliza swali kwa Meneja Miradi
wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo
kuhusiana na mradi huo wa Daraja la Kigamboni.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda (wa tatu kushoto)
akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa nne kushoto) wakati wajumbe wa kamati
hiyo wakitembelea Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es
salaam.

Waheshimiwa wakijadiliana wakati wa ziara hiyo.

Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau
(wa pili kulia mbele) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda alieambatana na ujumbe wake wakati
wakitembelea miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa
Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa
kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini
Dar es Salaam.

Maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.

Ubao wa Maelezo ya Mradi wa Kijiji

Wadau wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo.

Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau
akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.

Mh. Maua Daftari

Mh. Sugu.

Baadhi la Majengo ya Mradi wa Kisasa wa Dege eco Village yakiendele kujengwa.

Picha
ya pamoja ya Wabunge Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na
Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) mara baada ya
kumalizika kwa ziara.Picha zote na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment