Kaimu
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(aliyesimama) akizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wizara za
viwanda na biashara, fedha, uchukuzi, nishati na madini pamoja na
viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar.
Bibi
Maryam Khamis (Wapili kulia) Mtaalam wa uchumi kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Zanzibar akizungumza katika kikao hicho.
Pichani
ni baadhi ya viongozi waliohudhuria Kikao hicho. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt.
Adelhelm Meru.
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, Bw. Aunyisa Meena kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akichangia mada.
******************************************************
Na Saidi Mkabakuli
Wapanga
mipango nchini wameaswa kuzingatia weledi wakati wa kuandaa maandiko ya
miradi yanayowasilishwa kwa wafadhili ili kuongeza ushindani dhidi ya
nchi nyingine wakati wa uwasilishaji wa maombi ya kupatiwa ufadhili wa
miradi ya maendeleo.
Wito
huo umetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati alipofanya mazungumzo na viongozi
waandamizi kutoka wizara za viwanda na biashara, fedha, uchukuzi,
nishati na madini pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Zanzibar.
Bibi
Mwanri alisema kuwa kuna ushindani mkubwa kwa nchi zinazoomba ufadhili
wa miradi ya maendeleo hivyo uandishi wa maandiko yenye kuzingatia
weledi na viwango vya kimataifa ni msingi katika kuongeza ushindani na
kuweza kuwashawishi wafadhili kuvutiwa na miradi husika.
“Katika
kukabiliana na ushindani hatuna budi kujikita katika weledi na kuandika
maandiko yenye kuweza kuvutia wafadhili ili waweze kuja kuwekeza nchini
kwetu, ili tuweze kutimiza ndoto zetu za kuifanya Tanzania kuwa nchi
yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025” alisema Bibi Mwanri.
Mwezi
Juni mwaka 2011, Serikali iliandaa Mpango wa Kwanza wa Maeneleo
(2011/12 – 2015/16) kwa lengo la kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo
2025 ambapo Mpango huu ulihitaji takribani trilioni 40 ili kutekeleza
miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano.
Kwa mujibu wa Mpango huo, vyanzo vya utekelezaji wake ni pamoja na Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP); uwekezaji
wa kigeni; Hati Fungani kwa Waishio Ughaibuni; Hatifungani za ndani;
Hati Fungani katika Masoko ya Nje; Mifuko ya Pensheni na hifadhi ya
jamii; na makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi zinazoendelea.
No comments:
Post a Comment