Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wakimbizi 162,000 kutoka
Burundi waliopatiwa hati za uraia wa Tanzania katika ukumbi wa mkuu wa
mkoa wa Tabora jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati ya Uraia wa Tanzania
Bi.Bizimana Nyakiki Naluka, ambaye ni mmoja kati ya wakimbizi 162, 000
kutoka Burundi waliopatiwa uraia wa Tanzania katika hafla iliyofanyika
katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Tabora jana.
Baadhi ya Wakimbizi 162000 kutoka Burundi walipatiwa uraia wa Tanzania jana mjini Tabora.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya
Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao
vya CCM. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na watatu kushoto
ni Makamu wa CCm Bara Ndugu Philip Mangula.
Vijana wa CCM wa
mkoa wa Dodoma wakimvika skafu na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Dodoma ambapo anatarajiwa kuongoza vikao vya ngazi ya juu vya
CCM.
Rais Kikwete akikaribishwa na vijana wa ccm mkoa wa Dodoma, wakati akiwasili
mjini Dodoma akitokea mkoani Tabora mchana. Picha na Fredy Maro
No comments:
Post a Comment