Baadhi
ya Wanasalamu wa kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu njiro jijini
Arusha wakikabidhi sehemu ya msaada wao kwa uongozi wa hospitali ya
mkoa Mt.meru jana,kulia ni mratibu wa salamu kupitia kipindi cha usiku
wa moto Yacob Simba kushoto ni Sista Shubi Mjawizi,anayefatia ni Sista
Merry Stalla
Yacob Simba akiongea na baadhi ya wanasalamu katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru anayefatia ni Godfrey
Thomas ambao ni waratibu wa shughuli hiyo kupitia kituo cha Redio 5
katika kipindi usiku wa moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi
kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima
Yacob
Simba akikabidhi ndoo ya mafuta kwa uongozi wa hospitali ya Mt.Meru
jana baadaa ya wanasalamu kutoka mikoa zaidi 21 kufika hospitalini hapo
kuwafariji wagonjwa
Vicky
Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya Tan Communication
Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha,katikati ni Yacob Simba na Godfrey Thomas wakiwa wanajadili jambo
Kulia ni Lucy Bongole ambaye ni mwanasalamu wakiwa wanajadiliana na wenzake katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru katikati ni Zuhura Mbise maarufu kwa jina la mama Sosy,kushoto ni Sister Monduly
Kulia ni Lucy Bongole ambaye ni mwanasalamu wakiwa wanajadiliana na wenzake katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru katikati ni Zuhura Mbise maarufu kwa jina la mama Sosy,kushoto ni Sister Monduly
Wanasalamu wakiwa wanajadiliana
Sehemu ya msaada uliotolewa na wanasalamu kwa wagonjwa hospitali ya
Mt.Meru jijini Arusha
Kushoto
Mtangazaji maarufu wa Redio 5 kupitia kipindi chake cha love cuts
kinachorushwa jumatatu hadi ijumaa saa nne hadi saa saba usiku
Semio Sonyo akiwa na mtangazaji machachari aliyejizolea umaarufu mkubwa
kupitia kipindi chake cha usiku wa Moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima Godfrey Thomas aka GT wakifurahia jambo
Nesi
wa hospitali ya Mt.Meru Sista Merry Stella akitoa neno la shukrani kwa
wanasalamu waliofika kuwatembela wagonjwa hospitalini hapo ambapo
amewataka watu na mashirika mbalimbali kuiga mfano huo kwa kuwa mahitaji
ya wagonjwa ni makubwa
Muonekano katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
Wanasalamu wakiwa wamevalia T-sheti za Redio 5
Wapili kulia ni mmiliki wa jamiiblog Pamela Mollel wakwanza kushoto ni Godfrey Thomas aka GT wakiwa katika picha na baadhi ya wanasalamu jana zoezi hilo liliratibiwa na kituo cha Redio 5 kupitia kipindi cha usiku wa moto
Baadhi ya wanasalamu wakisubiria kuingia katika wodi mbalimbali kuwajulia hali wagonjwa hospitalini
hapo
"Pole mama Mungu atakuponya"hayo ni maneno ya wanasalamu
Yacob Simba mtangazaji wa Redio 5 akiwa anamjulia hali mama mgonjwa katika wodi ya
wanawake
Mwanasalamu
mkongwe kutoka Arusha Baba Ali Mbondei(aliyevalia tisheti ya Redio
5)akiwa na wanasalamu wenzake wakimjulia hali mgonjwa katika wodi ya
wanaume
Wanasalamu wakiwa wanasoma dua kwa mgonjwa wodi ya wanaume katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
Wanasalamu wakiwa wanaingia wodi ya saba
kuwaona wagonjwa
Godfrey Thomas
aka GT katikati akiwa amepozi na mashabiki wake ambao ni wanasalamu
kupitia kipindi cha usiku wa moto cha kituo cha Redio 5 jijini Arusha
No comments:
Post a Comment