Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga, Mama Fatma Karume akipitia mkataba walioingia na Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Fatma Karume kadi namba moja ya mfumo wa kieletroniki 'Gold Premium Card' mara baada ya benki hiyo kuingia mkataba wa kutengeneza kadi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay. (katikati)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla hiyo.
NA CLEZENCIA TRYPHONE
BENKI
ya CRDB imeingia mkataba na klabu ya Yanga kwa ajili kutengeneza kadi
za kisasa za uanachama wa klabu hiyo, ambazo pia watazitumia kuingilia
viwanjani katika mechi mbalimbali za mfumo wa tiketi za kieletroniki.
Yanga
imefikia hatua hiyo, kwa lengo la kuitafutia klabu vyanzo vya mapato
kwa ajili ya kujiendesha, ili iweze kufikia hatua nzuri zaidi kama
ilivyo kwa timu kubwa kama TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo
na nyinginezo.
Akizungumza
katika hafla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa benki hiyo, Dk.
Charles Kimei, alisema kuwa mkataba huo ni wa kudumu, ila utaweza
kuvunjwa endapo mambo yakienda tofauti na makubaliano.
Kimei
aliyasema hayo, katika zoezi hilo lilishuhudiwa na Fatma Karume ambaye
ni Mwenyekiti katika Bodi ya wadhamini wa Yanga aliyeweka sahihi katika
mkataba huo, pamoja na Francis Kifukwe na Makamu Mwenyekiti wa Yanga
Clement Sanga.
Akizungumza
kwa niaba ya Yanga, Fatma alisema, wao kama timu kongwe hapa nchini,
imefarijika kuona benki kubwa kama hiyo ikiwapa sapoti kubwa, ambapo
yeye amepewa kadi namba moja.
“Tunafarijika
sana, sisi kama Yanga kupata udhamini huu mnono, na Yanga ni taasisi
kubwa na ndio maana hata bendera za Taifa zinafanana na rangi ya klabu
yetu, sio hao Simba damu tu,”alisema.
No comments:
Post a Comment