Mafuta kwa Kituo.
|
Vijana
wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la
Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza katika picha ya makabidhiano na
wadau wa Airtel.
|
"Hawa ni watoto wetu, hivyo tunapaswa kuwalinda" Kauli ya pamoja ya wadau wa Airtel kwa wale wote wenye mapenzi mema.
|
Twaha bin Bakari Utari ambaye ni Katibu
mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA) ambao
ni wamiliki na kituo ameshukuru kwa msaada huo toka Aitel huku
akihamasisha wadau wengine kuiga mfano huo kwa ustawi wa jamii ya
Watanzania.
|
Sambamba
na kuzibainisha changamoto wanazokabiliana nazo kama vitabu,
madaftari,magodoro na sehemu za kulala, msimamizi wa kituo Al-Hajji
Hussein pia naye alikuwa na yake ya kusema.
|
Ahmad Mustapha ni mmoja kati ya vijana wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake.
|
Shumbana Hassan ni mmoja kati ya watoto wa kike wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii
imeanza kutoa futari katika vituo vinavyolea watoto waliopo katika
mazingira magumu nchini.
Kupitia
mpango huu Airtel imetoa msaada wa chakula kwa kituo cha Sharif Saidi
Al-Bath kinacholea watoto yatima kilichopo Nyegezi Majengo Mapya Jijini
Mwanza
Akiongea wakati wa kukabithi msaada huu , Meneja wa Kanda ya Ziwa wa
Airtel Bwana Raphael Daudi alisema” Airtel Kwa kutambua changamoto
nyingi zinazozikumba jamii tumeonelea ni vyema katika mfungo huu wa
ramadhani kutenga muda wa kutembelea na kutoa msaada kwa vituo
mbalimbali vya watoto yatima nchini. Leo tumetembelea kituo hiki cha
Sharif Saidi Al-Bathi na kuwapatia msaada wa chakula ambacho kitawasaidi
hata baada ya mwezi wa ramadhani.
lengo
letu ni kuhakikisha tunagusa mahitaji ya jamii kwa ujumla, husasani
watoto kupitia vituo vinavyowatunza huku tukihakikisha tunarudisha faida
tunayoipata kwa kuwafikia watanzania wengi kupitia shughuli zetu za
huduma kwa jamii kila mwaka.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath bwana Alhaji
Hussein Mussa Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu,
tumefurahi sana na kuona kumbe watanzania wenzetu na mashirika
mbalimbali wanaunga mkono jitihada zetu katika kuhakikisha tunawalea na
kuwasomesha watoto yatima. Kituo chetu bado kina mahitaji mengi hivyo
natoa wito kwa taasisi zingine kujiunga na kuendelea kusaidia kituo
chetu na vituo vingine nchini
Baadhi
ya watoto wanaoishi katika kituo hiki wameishukuru Kampuni ya Airtel
kwa msaada wa vitu mbalimbali walivyotoa na kuyatala makampuni mengine
kuiga yale yaliyofanywa na kampuni hiyo.
Vituo
vingine vitakavyopata msaada kutoka Airtel ni pamoja na New Hope
Family group-Temeke, Al-Hidaya children’s Home-ilala, Irishad
Madrasah-Mbezi kwa Msuguri (kinondoni), Kiboa orphanage-Arusha na
Heartfelt orphanage care Mbeya
Kituo
cha Sharif Saidi Al-Bath chenye watoto Yatima zaidi ya 50 kilichopo
Mwanza tayari kimepokea msaada kutoka Airtel mwishoni mwa wiki.
|
No comments:
Post a Comment