Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiangalia
mandhari ya mji wa Pangani wakati wa ziara ya kikazi wilayani
humo.Sehemu kubwa ya mji huo imo katika hatari ya kumezwa na bahari
kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali imeahidi kujenga ukuta
pembezoni mwa mto Pangani ili kuzuia athari za kimazingira kutokana na
kuongezeka kwa kina cha maji.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya hotuba zake akiwa ndani ya
kivuko kipya cha MV Pangani II wakati akivuka mto Pangani kutoka Tarafa
ya Bweni kuelekea Pangani mjini wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani
Pangani (Jumamosi).Rais Kikwete ambaye alikuwa mkoani Tanga kwa
ziara ya kikazi ya wiki moja alihitimisha ziara hiyo jana ambapo pamoja
na mambo mengine alisema kuwa serikali itajenga kivuko kingine kwenye
mto huo chenye uwezo mkubwa zaidi ili kuboresha shughuli za kiuchumi na
kijamii wilayani humo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya majumuisho wakati
akihitisha ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoani Tanga ambapo
alizindua na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo.picha na Freddy
Maro
No comments:
Post a Comment