Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania wakiwasili katika kituo cha kulelea watoto yatima
cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, jijini Dar es salaam. Vodocom
ilitemebela kituoni hapo kukakidhi hundi ya Sh. 20 kutoka Vodacom
Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji unaondeshwa na kituo
hicho.
Mkuu
wa Idara ya Huduma kwa Jamii wa Vodafone Laura Turkington akiwa na
watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Mwandaliwa wakifurahia picha kupitia
simu ya mkononi ya Laura. Wafanyakazi wa Vodacom walitembelea
kituoni hapo kukakidhi hundi ya Sh. 20 kutoka Vodacom Foundation
kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji unaondehswa na kituo hicho
Mkuu
wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano ya Vodacom Rosalyn Mworia akigawa
vitabu vya kujifunzia mambo mbalimbali vilivyochangwa na wafanyakazi wa
Vodacom kusaidia watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa. Mbalina
vitabu na vifaa vya kuchezea, Vodacom Foundation nayo ilikabidhi Sh 20
Milioni kusaidia mradi wa ushinjai na ufugaji wa kituo hicho.
Mkurugenzi
wa Kituo cah mwandaliwa Islami cha Bunju jijini Dar es salaam Halima
Ramadhan akiipitia kwa umakini mfano wa hundi mara baada ya kukabidhiwa
na wafanyakazi wa Vodacom. Fedha hizo zimetolewa na Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushinjai na ufugaji wa kituo hicho.
Mfanyakazi
wa Vodacom Tanzania Mariam Abdallah akiwafundisha kusoma baadhi ya
watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa vilivyotolewa na wafanyakazi
wa kampuni hiyo ikiwemo pia vitabu. Mbali na vitu hivyo, wafanyakazi ho
walikabidhi hundi ya Sh 20 Milioni iliyotolewa na Vodacom Foundation
kusiadia mradi wa ushonaji na ufugaji kituoni hapo.
======= ======= =======
Yatima Kituo cha Mwandaliwa wawezeshwa kuanzisha mradi wa kujipatia kipato
Dar es Salaam, Julai 1, 2014 … Kituo
cha Kiislamu cha kulelea watoto yatima na ushauri cha Mwandaliwa
Islamic Orphans Home and Counseling Support (MIOCA’S) kilichopo Mbweni
jijini dar es salaam kimepokea Sh 20 Milioni kutoka Vodacom Foundation
kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji ili kujijenga kiuchumi.
Fedha
hizo zimekabidiwa kituoni hapo wakati na wafanyakazi wa Vodacom
waliotembelea kituo hicho kwa lengo la pmaoja na mambo mengine
kuwaislisha pia Zawadi mbalimbali walizozikusanya wka ajili ya watoto
wanaelelewa kituoni hapo.
Akikabidhi
hundi ya fedha hizo kwa niaba ya Vodacom Foundation, mmoja wa
wafanyakazi wa kampuni hiyo Angela Mwakasege amesema Vodacom kupitia
mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation wakati wote inaguswa
na changamoto zinazoizunguka jamii ikiwemo suala la watoto yatima na
waishio kwenye mazingira magumu.
Amesema
hatua ya kukabidhi fedha hizo pamoja na zawadi za vitabu na vifaa
mbalimbali vya kuchezea watoto ni kielelezo cha jinsi ambavyo
wafanyakazi na kampuni kwa ujumla inayoguswa na kusukumwa kusaidia jamii
na kuweka mbele ajenda ya kusaidia kukabiliana na changamoto hizo
“Leo
tunafuraha sana kufika hapa, tunawapenda sana na tunaimani kwamba hiki
tunachpowakabidhi kitawasaidia kutimiza lengo lenu la kujijengea uwezo
wa kiuchumi kupitia miradi mnayokusudia kuianzisha ya ushonaji na
ufugaji.”Alisema Mwakasege
“Kwa
niaba ya wafanyakazi wote wa Vodacom kipekee tunawpongeza sana walezi
na viongozi wa kituo hiki kwa namna mlivyokubali kujitoa kuwalea watoto
hao. Sisi tunatambua kuwa hiyo sio kazi rahisi, tunawatia moyo mzidi
kujitoa kwa ajili ya akzi hii.”Alisema
Kituo
hicho chenye watoto 94 kinatarajia kuanzisha miradi ya ushonaji na
ufugaji itakayotumika kukiwezesha kituo kuwa na vyanzo vya mapato na pia
kuwa na fursa ya kuwajengea uwezo wa stadi za kazi na kujiajiri watoto
ili kuwapa uwezo wa kujitegemea katika siku za usoni.
Kwa
sasa kituo hicho kinajiendesha kwa kutegemea misaada ya wahisani
mbalimbali, lakini kuanzishwa kwa mradi huo wa ufugaji kuku wa nyama na
ushonaji kutawezesha kituo hicho kuounguza utegemezi wa wahisani.
Akisoma
maelezo ya kituo na shukrani kwa Vodacom Foundation na wafanyakazi wa
Vodacom kw akile walichowawezesha, Katibu wa kituo hicho Omary Ramadhan
amesema watoto walio wengi hupatikana kwa kuletwa kupitia Ofisi za
Ustawi wa Jamii wilaya ya Kinondoni na husomeshwa na wengi wao wapo
katika ngazi mbalimbali za elimu kuanzia ya chekechea.
Akizungumzia
msaada huo, xx alisema “ Tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu na
baadae kukubalika kwa ombi letu ka kusaidia fedha kufadhili mradi wa
ufugaji na ushonaji. Tunajua haikuwa kazi nyepesi, tulihataji kuwa
wavumilivu lakini hatiame tuanshukuru sana kuona leo tunaelekea kutimzia
ndoto yetu ya kuwa na miradi ya kiuchumi.”
No comments:
Post a Comment