Cheti hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam jana, mbele ya
wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa Kimataifa kutoka Uingereza,
Andrew Rowe, kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Mkoma (pichani).
“Cheti tulichopata leo chenye namba ISO 900:2008 ni kutokana na juhudi
za wafanyakazi wote wa TCRA za kuhakikisha tunatoa huduma bora
zinazokidhi haja za wateja wetu. Tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili
kutetea cheti hicho ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof.
Mkoma.
Akizungumzia cheti hicho, TCRA, Mhandisi kutoka Shirika la Viwango
Tanzania (TBS), Salvatory Rusimbi, alisema kinatokana na viwango bora
vya kazi, uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali zinazo tumika
kunufaisha utendaji kazi.
“Mkaguzi wa kimataifa amekuja hapa kutoka nchini Uingereza kutoa cheti
hicho cha kiwango kinachotokana na utendaji bora wa kimataifa ambao pia
unawanufaisha wateja na utendaji wa mamlaka hii, hii inaonyesha wazi
kuwa utendaji kazi wa TCRA ni bora zaidi,” alisema Rusimbi.
No comments:
Post a Comment