MICHEZO KIMATAIFA : MCHEZAJI WA UBELGIJI MWENYE ASILI YA KENYA ,DIVOCK ORIGI AJIVUNIA KUWA MKENYA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Jun 2014

MICHEZO KIMATAIFA : MCHEZAJI WA UBELGIJI MWENYE ASILI YA KENYA ,DIVOCK ORIGI AJIVUNIA KUWA MKENYA


Divock Origi
  Mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi akihutubia wanahabari Juni 13, 2014 nchini Brazil. Picha/AFP 

Baada ya Divock Origi kusaidia Ubelgiji kufuzu kwa kundi H kwenye dimba la dunia kule Brazil, mchezaji huyo amesema anajivuna kuwa Mkenya licha ya kuliwakilisha taifa jingine kwenye soka ya kimataifa.

RIO De JANEIRO, Brazil.
BAADA ya Divock Origi kusaidia Ubelgiji kufuzu kwa kundi H kwenye dimba la dunia kule Brazil, kwa bao la kipekee alilotia kimyani dhidi ya Urusi hapo Jumapili, mchezaji huyo alisema anajivuna kuwa Mkenya licha ya kuliwakilisha taifa jingine kwenye soka ya kimataifa.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Lille, Ufaransa , mwenye asili ya Kenya ambaye ana  uraia wa Ubelgiji, alipachika bao hilo la pekee kunako dakika ya 88 baada ya kuingia kama nguvu mpya mahala pa Romelu Lukaku, na kisha kuandaliwa pasi murwa na kiungo wa Chelsea, Eden Harzad.
“Pamoja na kwamba naichezea taifa la Ubelgiji katika soka ya kimataifa, sio siri kwamba naijivunia kuwa Mkenya kwani ndio mizizi halisi ya asili yangu. Bao lile nimelielekezea Wabelgiji wote kwa kunikuza na vile vile Wakenya ambalo ndilo taifa la wazazi wangu,” Origi alinukuliwa.
Bao hilo la dakika za majeruhi za mchuano huo ndio iliyoiwezesha Ubeljiji kufuzu kwa hatua ya timu 16 bora kwenye kundi H kwa kuzoa jumla ya alama sita. Hii ni baada pia ya kuandikisha ushindi mwingine kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Algeria waliowalaza 2-1. Sasa wamesalia na mechi moja dhidi ya Korea Kusini na hata ikiwa watapoteza, tayari wamefuzu kwa duru ya pili. Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, Korea Kusini waliotoka sare ya 1-1 na Urusi kwenye mechi ya awali, walilimwa 4-2 na Algeria.
Baada ya kuhangaishwa sana na Urusi pamoja na kucheza kwenye joto kali,  Origi aliipata nafasi ya kuvurumsha kombora nzito hadi kimyani zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kuisha, kufuatia mashambulizi ya kaunta alipopokea pasi nzuri yake Hazard kutoka kushoto mwa kisanduku cha wapinzani.

Mahojiano
Straika huyo mwenye umri wa miaka 19, ni mwanawe Mike Okoth, mshambuliaji na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.
Akifanyiwa mahojiano na kituo hicho cha BBC kuhusu hatua ya mwanawe kuichezea Ubelgiji badala ya Kenya, mkongwe Okoth alikuwa na haya ya kujibu.
“Baada ya ushauri wa kutosha, aliamua kuichezea Ubeljiji kwa kuzingatia masuala mengi; kama vile usimamizi mzuri wa kandanda nchini humo taofauti na ilivyo Kenya. Isitoshe ni Ubelgiji ambapo alikuza kipaji chake akiichezea katika viwango vyote kuanzia soka ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16, 17, 19 na sasa 21,” alisema.
Kingine kikubwa kilichomfanya kukataa kuiwakilisha Kenya ni kiwango cha soka cha Kenya ambacho kipo chini na vile vile hatua ya Ubelgiji kufuzu mara kwa mara kushiriki dimba la dunia tofauti na Kenya.
“Isitoshe baada ya mimi kuichezea Harambee Stars kwa muda mrefu, ninfahamu bayana changamoto chungu nzima zinazoikumba na kwa sababu Kenya haijulikani ni lini itafuzu kwa dimba la dunia, nilimshauri mwanangu kuichagua Ubelgiji,” aliongeza. Chanzo : Taifa Letu

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad