MAPISHI, CHEF KILE : SOMA HAPA NDIZI NYAMA ZINAVYOPIKWA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 25 June 2014

MAPISHI, CHEF KILE : SOMA HAPA NDIZI NYAMA ZINAVYOPIKWA




Naam leo njoo tupike ndizi nyama. Nimeona nishirikiane nanyi leo katika kuonyesha namna nzuri ya kupika ndizi nyama.
MAHITAJI
  • Ndizi (ndizi bukoba ndio zinafaa)
  • Vitunguu 2 vikubwa
  • Nyanya 4
  • Carrots
  • Binzali nusu kijiko cha chai
  • Mixed herbs
  • Rosemary
  • Pure Ginger / Tangawizi
  • Black paper / Pilipili manga
  • Tui zito la nazi / Coconut cream
  • Nyama ya ng’ombe 1/2
  • Corinder /Giligilani na carrots
JINSI YA KUPIKA
Kwanza chemsha nyama yako na iive vizuri sana, Menya ndizi zako na uzioshe vizuri, Andaa vitunguu, nyanya, Carrots na hizi spice za kutumia. Weka sufuria yako jikoni na mafuta , kisha weka vitunguu maji wakati vinaiva weka spices, anza na mixed herb, kisha weka binzali kidogo, weka tangawizi, rosemary kidogo viunge kwa muda kidogo kisha weka nyanya ipike nyanya hiyo hadi iive kabisa.
Baada ya nyanya kuiva sasa ndio muda wa kuweka carrots ambazo bila shaka ushazikata kata, weka nyama na ndizi zako, ongeza maji au supu ya nyama kama unayo, funika acha vichemke kwa dakika 10.
mapishi ya ndizi nyama na nazi
Baada ya dakika 10 ndizi zitakuwa zimeiva na ni muda wa kuweka ile coconut cream / tui la nazi kisha koroga kwa muda ili tui lisikatike na baada ya hapo zipo tayari kwa kula. Ila upata uhondo kamili angalia video ya mapishi ya Hapa.
Enjoy

No comments:

Post a Comment