BRAZIL v/s CHILE
Mshindi kati ya Brazil na Chile, atacheza na Msindi wa kati ya Colombia na Uruguay
2:- JUNI 28, MJINI RIO DE JENEIRO
COLOMBIA v/s URUGUAY
**************************************************
3:- JUNI 30, MJINI BRASILIA
UFARANSA v/s NIGERIA
4:- JUNI 30, MJINI PORTO ALEGRE
UJERUMANI v/s MSHINDI WA KUNDI H
********************************************************
5:- JUNI 29 MJINI FORTALEZA
UHOLANZA v/s MEXICO
Mshindi kati ya Uholanza na Mexico, atacheza na mshindi kati ya Costarica na Ugiriki
JUNI 29 MJINI RECIFE
COSTA RICA v/s UGIRIKI
JULAI 1 MJINI SAO PAULO
ARGENTINA v/S SWITZERLAND
JULAI 1
MSHINDI WA KUNDI H v/S MAREKANI
Na
Eleuteri Mangi-Maelezo
Mashindano
ya soka kombe la dunia yanaendelea kunoga na kupamba moto nchini Brazil
yakijumuisha jumla ya wachezaji 892 wanaoshiriki mashindano wa mpira wa miguu duniani
maarufu “Fifa World Cup” ya mwaka 2014.
Mashindano
hayo yamepambwa na majina ya wachezaji mbalimbali Mastaa kutoka nchi zinazoshiriki
kinyang’anyiro hicho kwa mwaka huu.
Kwa
mujibu wa mtandao wa FIFA, wachezaji wenye majina yenye herufi “M” ndio
wanaoongoza kwa idadi kubwa katika michuano hiyo ambao jumla yao ikiwa ni 85.
Miongoni
mwa wachezaji hao ni mshambuliaji Lionel Messi kutoka Argentina, Thomas Mülar
kutoka Ujerumani,John Obi Mikel kutoka Nigeria, Hossein Mahini kutoka Iran
na wachezaji wengine kutoka mataifa
yanayoshiki finali hizo.
Majina
mengine 807 ya wachezaji yapo katika herufi “A” hadi “Z” ukiyatoa yale ya herufi
“M” ambapo herufi A wapo wachezaji 68, B
69, C 57, D 56, E 21, 25, G 47, H 40, I wachezaji 17, J 42, K 42, L 30, N 17, O
23, P 40 na Q mchezaji mmoja, R 43, S 70, T 19, U wachezaji watano, V 37, W, 16,
X wachezaji wawili, Y na Z wachezaji 10.
Katika
mashindano hayo kuna jumla ya nafasi 736 za wachezaji ambapo kuna magolokipa
96, walinzi 230, walinzi wa kati 250 na washambuliaji 160.
Wachezaji
hao wanatoka katika timu za mataifa ya Algeria, Argentina, Australia, Ubelgiji,
Bosnia na Herzegovina, Brazil, Cameroon,
Chile, Colombia, Costa Rica, Ivory Coast, Croatia, Ecuador, Uingereza,
Ufaransa, Ujerumani, Ghana.
Mataifa mengine yanayoshiki fainali hizo ni Ugiriki,
Honduras, Iran, Italia, Japan, Jamuhuri ya Korea, Mexico, Uholanzi, Nigeria,
Ureno, Urusi, Hispania, Switzerland, Uruguay na Marekani.
Wachezaji hao wanaounda timu za mataifa
yao kwa kutokana na uraia wao aidha wa kuzaliwa au kujiandikisha na wanacheza
mpira katika vilabu mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa mtandao
wa FIFA, wachezaji 14 wanazechezea timu ya Bayern Muenchen, wachezaji
14 wanazechezea timu ya Manchester United, 13
Barcelona, 12 Chelsea, 12 Juventus, 12
Real Madrid, 12 SSC Napoli, 10
Liverpool, 10 Manchester City, 10 Paris
Saint-Germai na wachezaji 10 wanachezea
timu ya Arsenal.
Vilabu
vingine vilivyotoa wachezaji wanaoshiriki faina hizi ni
Atletico Madrid wachezaji 9, FC Porto wachezaji 9, FC Internazionale
wachezaji 8, AC Milan wachezaji 8, Schalke 04 wachezaji 7, FC Zenit
St.
Petersburg wachezaji 7, FC Dynamo Moscow
wachezaji 7, SS Lazio wachezaji 7, Southampton FC wachezaji
7, VfL Wolfsburg wachezaji 7, Tottenham Hotspur wachezaji 6, Newcastle
United wachezaji 6, FC Basel wachezaji
6, Everton wachezaji 6, CSKA Moscow wachezaji
6, Borussia Dortmund wachezaji 6, AS
Roma wachezaji 5, Feyenoord Rotterdam wachezaji 5, Fenerbahce SK
wachezaji 5, FSV Mainz 05 na Galatasaray SK zote zimetoa wachezaji
watano kila mmoja.
Ili
kuhakikisha timu za mataifa hayo zinakuwa na mafanikio wapo jumla ya makocha 32
wa timu za mataifa hayo ambao wanaongoza benchi la ufaundi kwa timu zao.
Fainali mwaka huu zilianza 12 Juni na zinatarajiwa
kuhitimishwa Julai 13 kwa kwa mechi ya fainali ambayo itaamua nani atatawazwa
kuwa mwamba wa soka duniani baadya ya bingwa mtetezi Hispania kutolewa mapema
katika mzunguko wa kwanza wa mashindano haya.
Mpaka
sasa hadi kufikia kipindi hiki cha hatua ya pili ya timu 16 bora, miamba
iliyofanikiwa kupenya katika hatua hiyo kutoka kundi A ni Brazil na Mexco,
kundi B Uholanzi na Chile, kundi C ni Columbia na Ugiriki, kundi D Costa Rica
na Uruguay, kundi E ni Ufaransa na Swirtzerland, kundi F ni Argentina na
Nigeria, kundi G ni Ujerumani na Marekani na kutoka kundi H timu zilizopenya ni
Ubelgiji na Algeria.
Kigenga cha hatua ya timu 16 bora kitapulizwa Juni 28
mwaka huukwa timu ya wenyeji wa mashindano Brazil kuvaana na Chile.
Timu
nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni Columbia ambao watacheza na Uruguay, Uholanzi
watacheza na Mexco, Costa Rica watacheza na Ugiriki, Ufaransa watacheza na Nigeria,
Ujerumani watacheza na Algeria, Argentina watacheza na Swirtzerland na kipenga
cha mwisho katika hatua hii kitakuwa kati ya Ubelgiji ambao watavaana na
Marekani hapo Julai Mosi mwaka huu katika dimba la Arena Fonte Nova, Salvador
nchini Brazil.
Mataifa
yaliyofuzu kushriki fainali za mwaka huu ni 32, ambapo imekuwa na fainali ya 19
tangu kuasisiwa kwake mwaka 1930. Mataifa hayo yanatoka katika bara la Africa, Asia,
Amerika ya kaskazini, Amerika ya kusini, Oceania na Ulaya.
No comments:
Post a Comment