Viongozi
wa Mtaifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakilizindua Mnara
wa kumbumbuku ya mauaji ya Rwanda yaliyotokea karibu miaka ishirini
iliyopita hapo Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Arusha Tanzania.vKutoka
kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza, Rais
Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Rais wa Kenya mabae pia ni Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo Rais Uhuru Kenyata, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na
Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana PierreDamieni Habumuryemi.
Wakuu
waJumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya kumalizika kwa Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha Tanzania.Kutoka
Kushoto waliokaa vitini ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza, Rais
Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Rais Yoweri
Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni
Habumuryemi.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwapongeza Majaji wapya wa Mahkama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
waliokula kiapo kwenye Mkutano wa 12 wa kuitumikia Jumuiya hiyo Mkoani
Arusha. Nyuma yake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Wakuu
wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha
Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa
Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha { AICC }.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa
Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.
Baadhi
ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha. Wa
mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla
Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri
wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyeta wa Kenya akihutubia Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha.
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini baadhi ya hati za makubaliano ya Jumuiya hiyo. Kutoka
kulia ni Rais Wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya ambae ndie
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Uhuru Kenyata, Rais wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana
Bazombaza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiimba wimbo Maalum wa Jumuiya hiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha { AICC }.
Majaji wapya walioapishwa kushika nyadhifa mbali mbali kwenye Mkutano wa 12 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha. Kutoka Kushoto ni Jaji Edward Mtakangwa, Dr. Anon Regerwa na Jaji Fakih Jundu.
<<<<<<<<<< >>>>>>>>>
Na Othman Khamis Ame
Mataifa
wanachama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yanapaswa kuzingatia
umuhimu wa ulinzi wa pamoja wa eneo lote la Afrika ya Mashariki kwa
lengo la kujaribu kudhibiti vitendo vya ugaidi vinavyoonekana kujitokeza
katika baadhi ya Nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyata wa Jamuhuri ya Watu
wa Kenya alieleza hayo wakati akiuhutubia Mkutano wa 12 wa siku moja wa
Viongozi Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa
Arusha (AICC).
Rais
Uhuru Kenyata alisema Mataifa ya Afrika Mashariki hasa pembe ya Bara
hilo imekumbwa na wimbi la vitendo vya kigaidi kiasi kwamba huleta hali
ya wasi wasi kwa wakaazi wa eneo hilo.
Alisema ukosefu wa utulivu katika baadhi ya maeneo ndani ya ukanda wa
Bara la Afrika umekuwa ukiipa wakati mgumu jumuiya hiyo kiasi kwamba
Mataifa wanachama yanalazimika kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana
na tatizo hilo.
“
Ukanda wa Afrika Mashariki umekuwa ukikumbwa na vitendo vya kiharamia
pamoja na ugaidi jambo ambalo halileti sura nzuri kiasi kwamba huchangia
hali ya wasi wasi kwa wana Jumuiya wote “. Alifafanua Rais Uhuru
Kenyata.
Akizungumzia
suala la kuwa na Ushuru wa Forodha na Soko la pamoja la Jumuiya ya
Afrika Mashariki Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya hiyo Rais Kenyata alisema
upo muelekeo mzuri wa suala hilo ambalo linaonekana kupewa Baraka na
Viongozi wa Mataifa wanachama.
Rais
Uhuru Kenyata alifahamisha kwamba taratibu na mikakati ya kisheria
imekuwa ikiendelea kuchukuliwa na watendaji pamoja na Wataalamu wa
Jumuiya hiyo ili kuona suala hilo linafikia muwafaka.
Alieleza
kuwa juhudi za kuwa na ushuru wa forodha na soko la pamoja la Jumuiya
ya Afrika Mashariki zilizoanza harakati zake kati ya mwaka 2005, 2010
na 2013 zimelenga kustawisha hali ya uchumi ya wananchi wa mataifa
shirika wa Jumuiya.
Mwenyekiti
huyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki { EAC } aliipongeza Tanzania kwa
kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ulioasisiwa na Mataifa mawili huru ya
Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Rais
Kenyata alisema kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
imekuwa kielelezo cha kihistoria ndani ya Bara la Afrika pamoja na
Mabara mengine Duniani.
Alieleza kwamba Afrika Mashariki na Bara zima la Afrika limepata heshima
kubwa katika Nyanja za kisiasa kutokana na Muungano wa Tanzania
uliofikia nusu karne sasa tofauti na ile miungano mengine iliyoshindwa
kumudu hata kwa miezi michache.
Mapema
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera
ameishukuru Tanzania chini ya Rais wake Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
ukarimu wa Wananchi wake.
Balozi Dr. Richard Sezibera ukarimu huo unaoendelea kuviwezesha vikao
mbali mbali vya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika kazi zake za
kila siku Ndani ya ardhi ya Tanzania.
Katika
Mkutano huo wa 12 wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Majaji Watatu waliapishwa kushika nyadhifa mbali mbali katika baraza la
Majaji la Jumuiya hiyo.
Majaji
hao ni pamoja na Mh. Edward Mtakangwa, Dr. Aron Regerwa, Jaji Fakih
Jundu akiwemo pia Dr. Enos Bukuku aliyeongezewa muda wa kuendelea kuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.
Halkadhalika
Viongozi hao Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa pamoja pia
walizindua Mnara wa kumbumbuku ya mauaji ya Rwanda yaliyotokea karibu
miaka ishirini iliyopita.
Mkutano
huo wa 12 wa Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umehudhuriwa
na Rais Uhuru Kenyata wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Mwenyeji wa Mkutano
huo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wengine
ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombasa, Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni pamoja
na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment