JESHI
la Polisi hapa nchini, limeshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa
madawa ya kulevya katika mkoa wa Manyara, ambapo kwa sasa Polisi
wamekamata misokoto ya bangi 2,676 na mirungi bunda 70 katika mkoa huo,
huku likishindwa kakabiliana na hali hiyo kutokana na Askari wake
kushiriki vitendo hivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Bangi1
Aidha
kumbukumbu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha Machi, mwaka 2012, Jeshi
hilo mkoani Kilimanjaro lilimshikilia Askari wake (G 842, Konstebo
Deogratius), ambaye alikamatwa na misokoto mine ya bangi akiwa katika
ukumbi wa disko wa Albeto uliopo mjijni Moshi, huku akifanya vurugu
katika ukumbi huo ambapo pamoja na Jeshi la Polisi mkoani humo
kuthibitisha tukio hilo, mtuhumiwa huyo akisukwa rumande pamoja na
Askari mwingine ambaye aliingia katika ukumbi huo akiwa na bunduki aina
ya SMG na kufanyia watu fujo.
Mbali
na matukio hayo Jeshi hilo, lilitoa taarifa ya kukamata kwa watuhumiwa
45 wakihusishwa na matukio ya utumiaji wa bangi, mirungi na gongo katika
msako wa kuimarisha doria katika maeneo mbalimbali mkoani humo, msako
ambao hadi leo Polisi mkoani humo wameshindwa kuwafikisha makahamani
watuhumiwa wakidai bado uchunguzi haujakamilika Globu ya Jamii imebaini.
bangi watuhumiwa
Misokoto 2,676 ya bangi yakamatwa
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Deusdedit Nsimeki, amemwambia Mwandishi wetu
kuwa Aprili 15 saa 11:30 asubuhi katika eneo la Minjingu barabara ya
Arusha-Babati, walimkamata, Nassoro Idd (27) mburege mkazi wa Singida
mjini akiwa na misikoto ya bangi 2000 akiwa anatumia usafiriwa basi la
kampuni ya Mtei lenye namba T.449 CAL, lililokuwa likitokea Arusha
kwenda Singida.
Amesema
siku hiyo hiyo huko minjingu Kata ya Nkaiti, Askari waliokuwa doria
walimkamata, Juma Khatibu (18) Mshilazi na mkulima wa Arusha, akiwa na
bangi misokatomo 620, iliyokuwa imehifadhiwa ndani ya mikate iliyokuwa
imetobolewa, ambapo mtuhumiwa alikuwa ni abiria wa basi la kampuni ya
Kandahar lenye namba T. 391 BUR lililokuwa likitokea Moshi kwenda mkoani
Singida.
Bangi msokoto
Aidha
Nsimeki, alisema katika Kata ya Nkaiti, wilayani Babati, Riziki Ferisi
(18) Mchaga na mkulima wa moshi alikutwa na bangi misokoto 56 akiwa
kwenye basi la Mtei lenye namba T.991 ABC, lililokuwa likitokea Moshi
kwenda Singida, ambapo Aprili 13 maeneo ya magugu, Edward Mollel (27),
Janeth Mollel (27 na Mudi Robert (33) kwa pamoja walikuwa wanasafirisha
madawa ya kulevya aina ya Mirungi bunda 70 yaliyokuwa kwenye gari aina
ya Noah yenye namba T.339 BYE, inayomilikiwa na Edward Mollel, mkazi wa
Singida.
“Pamoja
na kuwa kuna mbinu mpya zinatumika kusafirisha madawa haya, ikiwemo
kuweka kwenye siti za magari kama Noah,’Tyubu’ za matairi ya magari,
mifuko mbalimbali na mabegi, na kuweka ndani ya mikate iliyotobolewa
lakini bado tumegundua mbinu hizo” alisema Nsimeki.
Ameiambia
FikraPevu kuwa, Jeshi hilo limejizatiti kwa kuhakikisha kuwa hakuna
makosa ya uhalifu, yatakayovunja amani katika maeneo yote ya mkoa huo
katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka.
Walimiki wa mabasi kukumbana na mkono wa sheria
No comments:
Post a Comment