(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
SERIKALI
ya Tanzania imepokea msaada wa jumla ya Euro milioni 20 ambazo ni sawa
na sh. Bilioni 40 za Kitanzania uliotolewa na serikali ya Ubelgiji
kuisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi ya kilimo na maji.
Lengo
la msaada huo wa serikali ya Ubelgiji kwa serikali ya Tanzania ni wa
kusaidia sekta ya kilimo na maji kwa kuzingatia kilimo ni uti wa mgongo
wa nchi yetu na maji ni uhai kwa maendeleo endelevu taifa.
“Napenda
kuihakikishia serikali ya Ubelgiji kuwa msaada walitupatia utatumika
kwa manufaa ya watanzania wote kwa malengo yaliyokusudiwa” alisema Dkt.
Likwalile.
Akisisitiza
juu ya msaada huo Dkt. Likwalile alisema kuwa msaada ho umekuja muda
muafaka ambapo Tanzania inatekeleza Mpango wa Maendeleo Makubwa Sasa
(BRN) ambapo una manufaa ya kurekebisha huduma za jamii ikiwemo
kuwapatia wananchi maji safi na salama.
BRN ni dhana inayotekelezwa na serikali na kuonekana matokeo yake ni mazuri katika nchi nyingine.
Miongoni
mwa watakaonufaika na msaada huo ni wakazi wa Dar es salaam. Kigoma na
meneo ya vijijini na kuwapunguzia muda wa kutafuta maji umbali na muda
mrefu na hivyo kuwapa nafasi ya kutumia muda wao katika shughuli
nyingine za kiuchumi na kijamii na kupunguza umasikini kwa maendeleoya
taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Serikali ya Ubelgiji alisema kuwa uliotiwa
saini ni kiashiria na alama ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya serikali
nhizi mbili.
Kwa kudhihirisha Moors alisema kuwa serikali yake pia inasaidia asisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali.
Asasi
zinazonufaika na misaada inayotolewa na serikali ya Ubegiji ni pamoja
na Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA, Chuo kikuu cha Nelson Mandela, Chuo
Kikuu cha Mzumbe, VECO, DON BOSCO na TRAIAS.
Mkataba
uliosainiwa ni wa muda mfupi kwa miaka miwili 2014 hadi 2015ambao ni wa
mpito ambapo unaandaliwa mpango wa muda mrefu ambao ni wa muda mrefu
kuanzia 2015/2016 hadi 2019/2020
No comments:
Post a Comment