MTOTO WA MWANAHARAKATI WA MICHEZO NCHINI TANZANIA BW. WILHELM GIDABUDAY ASEMA "I HOPE I CAN KEEP THE NAME UP TO WHAT IT WAS!" AKIWA NCHINI MAREKANI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 7 October 2013

MTOTO WA MWANAHARAKATI WA MICHEZO NCHINI TANZANIA BW. WILHELM GIDABUDAY ASEMA "I HOPE I CAN KEEP THE NAME UP TO WHAT IT WAS!" AKIWA NCHINI MAREKANI


Sydney Gidabuday wakati akiwa mdogo
Sydney Gidabuday ni mwanariadha mzuri mzawa wa Marekani mwenye asili ya kitanzania aliyezaliwa na wazazi wake wote wawili (watanzania).

Wilhelm Francis Gidabuday ambaye ni baba mzazi wa Sydney, ni mzaliwa wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara hapa Tanzania. 
 Mwaka 1993 Gidabuday alipata udhamini (Scholarship) ya kwenda kusoma nchini Marekani ambapo pia baada ya mwaka moja Gidabuday alimfanyia mpango rafiki yake wa kike ili aende Marekani kutafuta elimu na maisha kwa ujumla. Lakini kadri siku zilivyozidi kusonga mahusiano yao na dada huyo ambaye pia ni mtanzania wa wilaya ya Hanang yalizidi kuwa makubwa na hata kufikia kuwa mke halali wa Wilhelm Gidabuday. 

Historia ikaanzia hapo. August 21, 1996 alizaliwa mototo wao waliomuita Sydney katika kituo cha (Riverside Community Hospital) kilichopo mjini Riverside jimbo la California nchini Marekani. 
Mtoto ambaye baba na mama yake ni watanzania waliokwenda huko kusoma lakini Mungu akawapa zawadi kubwa zaidi ambayo ndiyo mtoto Sydney. “Nilikuwa mwanafunzi wakati ule, nilikuwa na wakati mgumu sana maana kupata mtoto haikuwa ndani ya program iliyonipeleka Marekani, lakini ilibidi nikomae pande zote za kimasomo na kulea familia” alisema Gidabuday

Aliongeza kuwa “hata hivyo mungu ni wa ajabu maana yote yalikwenda salama na baadae tukaja na mtoto wetu Tanzania ambapo alikaa kwa miaka mitano akihodhi uraia wake wa Marekani kisheria, tukaamua kumrudisha California aweze kupata haki yake ya msingi ya kimasomo na afya kama raia halali wa Marekani”.
Gidabuday anazidi kueleza kuwa "Kuanzia mwaka juzi Sydney Gidabuday aliyepewa jina la Dambir na babu yake mzee Francis Gidagharomga Gidabuday, kwani amekuwa akionyesha dalili za kuwa mwanariadha ambaye Marekani haijapata kuwa naye kama mzaliwa wa ndani ya nchi. 
Jina la Dambir lina maana ya “kuruka” babu yake alitafuta jina zuri la kumpa akimaanisha mjukuu wake alifikaje Marekani wakati hakusafiri na chombo chochote?, baba na mama yake walikwenda kwa ndege; lakini yeye alifikaje huko?. 
Hivyo ukoo ukaridhia jina hilo apewe Gidabuday mdogo. Hivi sasa Sydney anamalizia mwaka wa mwisho katika El Modena Highschool iliyopo mji mdogo wa Orange uliopo kusini mashariki mwa mji mkubwa wa Los Angeles California
Anajitahidi sana na jina lake ni kubwa sana katika mashindano ya kishule jimbo la California na Marekani nzima. “Vyuo vikuu vingi vimeniandikia barua ya kumpa mtoto wangu Schorlaship, ila mimi nasubiri kwanza nichague shule bora zaidi na ambayo itamsaidia kupata program zote za elimu na michezo kwa pamoja” alisema Gidabuday

Wilhelm Gidabuday enzi zake pia alitingisha California nzima katika mashindano ya vyuo ambapo amepata kuwa State Champion katika Cross Country Championships mara mbili, pia amekuwa State track Champion katika mbio za uwanjani za mita 5,000 na 10,000 mara mbili na ameshawahi kupewa tuzo maarufu kabisa ya “State Athlete of the Year”. Hivyo mtoto wake (Sydney) anatamani kupata tuzo hiyo pia.
Pichani ni baba na mwana - kushoto ni SYDNEY na (kulia) ni baba yake Sydney yaani Wilhelm Gidabuday enzi hizo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Sydney Wilhelm Gidabuday aliandika ujumbe huu "I Hope I can keep the name up to what it was!" ulioambatanishwa na picha hiyo hapo juu. Kwa hisani ya Asili Yetu Tanzania Blog

No comments:

Post a Comment