TAMASHA LA TASWA KUFANYIKA KESHO KATIKA VIWANJA VYA GENERAL TYRE-NJIRO ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 7 September 2013

TAMASHA LA TASWA KUFANYIKA KESHO KATIKA VIWANJA VYA GENERAL TYRE-NJIRO ARUSHA

Katibu wa Taswa Arusha Bw. Mussa Juma akiongea na
waandishi wa habari kuhusiana tamasha la taswa linalotarajiwa
kufanyika kesho katika kiwanja cha general tyre


Na Woinde Shizza,Arusha

Tamasha la michezo la waandishi wa habari Taswa linatarajia kufanyika

kesho September nane katika viwanja vya general tyre  vilivyopo njiro
jijini hapa.

Akiongelea tamasha hilo katibu wa chama cha waandishi wa habari za

michezo mkoani arusha Musa Juma alisema kuwa maandalizi ya tamasha
hilo yamekamilika na jumla ya timu 12 zinatarajiwa kushiriki katika
tamasha hilo.

Alisema kuwa michezo mbali mbali itachezwa katika tamasha hili ikiwa

ni pamoja na kufukuza kuku,kukimbia na magunia,mpira wa miguu ,mpira
wa pete pamoja na michezo mingine mbalimbali sambamba na burudani
mbalimbali za muzikikutoka katika sehemu na bendi mbalimbali.

Alisema kuwa hili nitamasha la nane kufanyika na kwa mara hii

wameboresha zaidi kwani zawadi zimeongezeka tofauti na kipindi
kingine.

Amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza katika tamasha hili  kwani

tamasha hili ni lakihistoria  kutoka na waandishi mbalimbali kushiriki
kutoka katika mikoa mbalimbali.

Alitaja baadhi ya timu zitakazo shiriki katika tamasha hili kuwa ni

pamoja na timu ya taswa ya jijini dar es salaamu ambapo inatarajiwa
kuwasili leo timu ya taswa arusha ambao ni wenyeji wa bonanza
hili,timu ya taswa manyara ,timu ya triple a fm ,sunrise fm,radio five
pamoja na timu nyingine nyingi ikiwemo timu ya tbl ambao ni wathamini
wakuu pamoja na timu ya wazee klabu.
TASWA FC toka Dar Es Salaam, wakiwa safarini kuja Arusha Kwenye Bonanza la Vyombo vya habari utakao fanyika kesho  katika viwanja vya General Tyre-Njiro Arusha.

No comments:

Post a Comment