KATIBU MKUU WA CCM AKIWA KATIKA ZIARA YAKE, WILAYANI TARIME - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 24 September 2013

KATIBU MKUU WA CCM AKIWA KATIKA ZIARA YAKE, WILAYANI TARIME


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013..
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Nyamongo Chacha Magayo Butora ambaye alifafanua kwa kina matatizo yanayowakabili wakazi wa eneo hilo,Katibu Mkuu alitumia Demokrasia ya hali ya juu baada ya kuwapa nafasi watu watatu mbali mbali ambao wananchi waliwachagua waje kuelezea matatizo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani mara ambapo aliamua kufuta kila kitu kwenye ratiba yake na kutaka wananchi wateue wawakilishi wao ili wakakae kikao na watu wa serikali ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele akifafanua mambo kadhaa ambayo Wizara yake inataka wananchi wafaidike na migodi ikiwa pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo ambao wanatakiwa wajiunge kutengeneza vikundi. Kwa picha zaidi Bofya hapa >>>

No comments:

Post a Comment