PICHA MBALI MBALI:DKT. GHARIB BILAL AHANI MSIBA WA JAJI MSTAAFU BUXTON CHIPETA JIJIN DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 20 July 2013

PICHA MBALI MBALI:DKT. GHARIB BILAL AHANI MSIBA WA JAJI MSTAAFU BUXTON CHIPETA JIJIN DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa ndugu wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo, nyumbani kwa marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Majaji waliohudhuria msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, baada ya kuhani msiba huo wa Jaji mstaafu Buxton Chipeta.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waombolezaji katika msiba wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam ,kwa ajili ya kuhani na kuaga msiba huo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu katika msiba huo.Picha na OMR

No comments:

Post a Comment