Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiro amejibu maswali mbalimbali aliyoulizwa na Mtangazaji Salim Kikeke kutoka Crown Media.
Kikeke amemuuliza maswali mbalimbali Dk.Migiro ambayo kwa sehemu kubwa yalijikita katika ripoti ya Tume ya kuchunguza vuruga kabla na baada ya Oktoba 29 ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande.
Nakuletea maswali matano kati ya maswali mengi aliyoulizwa
Dk.Migiro na kuyajibu kwa ufasaha na weledi mkubwa.Majibu ambayo yanathibitisha uwezo na umahiri wake katika uongozi hasa kwa kutambua historia yake ya uongozi kitaifa na kimataifa.Maswali hayo yalikuwa hivi;

Kikeke:Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kimya kwa muda mrefu tangu ripoti ya Jaji chande kutoka, kwanini imekuwa kimya na kwanini sasa mmekubali kuzungumza na sisi?
Dk.Migiro: Ningependa kuliweka jambo hili katika muktadha sahihi , mtambuka vurugu za Oktoba 29 ni tukio ambalo lilitusitua wengi na sisi wana CCM tulishutuka zaidi kwani haijawahi kutokea katika taifa letu.
Tulipata mshangao, kulikuwa na kuduwaa na kulikuwa na kutafuta muda wa kulitafakari kwa kina nini kimetupata sisi Tanzania baada ya miaka mingi ya kuwa nchi yenye utulivu, amani na mshikamano
Kwahiyo ilichukua muda, na ilituhitaji kuitafakari hotuba ile ya Jaji Chande ambayo ilitokana na kazi waliyoifanya yeye na wana Tume wenzake.Kwahiyo ilichukua muda lakini baadae Chama kilizungumza kidogo kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi Kenani Kihongosi
Naye alisema wazi kwanza tunapongeza kuanzishwa kwa tume ile ilikuwa hatua muhimu katika kurejesha nchi yetu kwenye mstari.Pili alishukuru tume kwa kazi waliyofanya , kazi ambayo wameifanya kwa weledi mkubwa na mpaka sasa inaendelea kuwa sehemu ya namna ya sisi kubaini nini kilitokea na twendeje
Vilevile aliwashukuru wananchi , kwasababu kazi ya tume isingekamilika kama wananchi wasingejitokeza wakaunga mkono, wakatoa maoni yao.Kwahiyo ilikuwa hatua muhimu.
Lakini leo hii umetaka kuongea na sisi ni fursa nzuri na wakati muafaka na mimi Katibu Mkuu kueleza zaidi kuhusu muelekeo wetu kama Chama Cha Mapinduzi kuhusu taarifa ile twendeje kama Taifa na mengineyo ambayo utaona yanafaa
Kikeke:Umezungumza aliyosema Katibu Mwenezi,mnaunga mkono taarifa iliyotolewa na Tume ya Jaji Chande?
Dk.Migiro: Kwanza CCM tumepokea taarifa hii kwa umakini mkubwa na kwa kujua kwamba ni hatua muhimu sana tunataka kujua nini kilitokea kwasababu tunataka suala hili lisijirudie na Chama Cha Mapinduzi kingependa kufuatilia kwa karibu sana hatua gani zitafuata baada ya tume kutoa taarifa yake.Ni wakati muafaka kabisa kwa sisi CCM kuzungumza kupitia sauti ya Katibu Mkuu
Kikeke: Chama Cha Mapinduzi katika mkutano wake wa Halmashauri Kuu Taifa walionekana kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama katika matukio ya Oktoba 29 , watu waliuawa katika siku ile ,kwanini mlifanya vile?
Dk.Migiro:Kwanza kabisa niseme tunaendelea kuonesha masikitiko yetu makubwa sana kwa vifo vilivyotokea .Vinapotokea vifo au hata kifo kimoja ni suala zito .Katika taarifa yake Mheshimiwa Jaji Chande alieleza kwamba tume ilibaini kuna watu takribani 518 waliopoteza maisha pamoja na madhara mengine yamejitokeza.
Kwahiyo Chama Cha Mapinduzi tunachukua hili suala kwa masikitiko makubwa sana na wako wengine wanaosema idadi hiyo ni ndogo labda ingekuwa kubwa lakini tutakumbuka tume ilitueleza na sisi Chama Cha Mapinduzi hatuna sababu ya kutia shaka vyanzo vyao ndio viliwapa taarifa ile.
Walisema walipata taarifa kupitia hospitali binafsi ,hospitali za serikali, Msajili wa Vizazi na vifo.Zote hizi zimeonesha watu 518 ndio waliopoteza maisha lakini walitutahadharisha inawezekana idadi ile ikabadilika kwasababu wako ambao hawakwenda hospitali wala hawakuandikisha.Sasa kwa Chama Cha Mapinduzi uhai wa mtu mmoja ni uhai mkubwa ambao hatuwezi kupima kwa namba
Kwa maana hiyo tumesikitika sana. Sasa kuhusu vyombo vya ulinzi na usalama ndugu Kikeke unafahamu katika nchi yeyote na Tanzania haina tofauti ,vyombo vya ulinzi na usalama vina kazi zake, vina jukumu ,tukizungumzia Polisi mojawapo ya majukumu yake makubwa ni kulinda usalama wa raia na mali zao.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania linakazi kubwa ya kulinda mipaka ya nchi yetu,majukumu yake ya msingi ndio hayo sio kuua wananchi na tunafahamu tarehe 29 Oktoba nchi nzima tulikuwa na vituo vya kupigia kura takribani 99,000.
Na kwakuwa tuliamka katika hali ya kawaida wenzetu wanaolinda usalama wa raia walikuwa tayari wamekaa kwenye maeneo ya kupiga kura kwasababu wananchi waliowengi walikuwa wamejitayarisha kutoka kwenda kupiga kura na kurejea nyumbani.
Sasa ilipotokea kadhia ile vyombo hivi na hasa polisi walilazimika kujigawa huku usalama uendelee kuwepo kwenye maeneo ya kupiga kura na huku waje katika yale maeneo yaliyokuwa na fujo na pia itakumbukwa fujo hii ilikuwa kama moto wa nyikani , pale fujo huku fujo,sio Dar es Salaam peke yake ni katika nchi nzima kwa ujumla.
Kwahiyo hawa walikuwa kama wana jambo kubwa la kufanya kuhakikisha kura zinaendelea kupigwa na vile vile usalama katika maeneo mengine.Hilo lilikuwa jukumu lao kubwa na walilifanya na tunaamini kama wasingefanya vile labda madhara yangekuwa makubwa zaidi katika taifa letu.
Na pili ambalo naweza kuliunganisha hapo kwanini pia Chama Cha Mapinduzi kupitia halmashauri kuu tuliwapongeza. Kwasababu kazi waliyoifanya ndio imefanya taifa letu liwe imara mpaka leo pamoja na ile fujo ambayo kwanza hatukuitegemea lakini pia haijwahi kutokea.
Kwahiyo ilitushangaza wote tukapigwa na butwaa na kitu ambacho ningependa tutenganishe hapa inawezekana katika utendaji wa kazi zao kukawa na dosari hiyo inatokea, sasa tusichanganye majukumu yao ya msingi.Kazi nzuri waliyoifanya ya kutunza amani kwa kiwango kile ambacho kilihitajika kwa wakati ule na dosari moja moja zinazojitokeza…
Na hapa sisemi vifo ni dosari ndogo, sio dosari ndogo ni kubwa lakini ndio sababu kuna haja sasa ya kuangalia mazingira ya vifo vile lakini haindoi ukweli kazi waliyofanya ni ya kutukuka katika Taifa letu.
Kikeke:Mheshimiwa Katibu Mkuu inaonekana kama vile vyombo vya dola na hasa polisi vinaingia kwenye siasa kama kukilinda Chama Cha Mapinduzi ,kwanini?
Dk.Migiro:Hebu niambie siasa gani Jeshi la Polisi inafanya ikiashiria wanakilinda Chama Cha Mapinduzi?
Kikeke :Inaonekana kama inazuia wananchi wasitekeleze haki zao kwa kukitetea Chama.
Dk.Migiro:Si kweli ,kwanza kwa kuwa tunazungumzia masuala ya chaguzi ningependa kukumbusha katika mchakato wote wa uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano, iwe Bara au Zanzibar hakukua na hali ambayo Jeshi la Polisi ililazimika kuingia kutuliza fujo au kudhibiti waliokuwepo.
Hii inaonesha vyama vyote vilifanya shughuli zao kwa utulivu kabisa na utakumbuka Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya uzinduzi wa kampeni alisema tunataka tufanye kampeni za kistaarabu,za tulivu ili kuwapa wananchi fursa ya kusikiliza Ilani ya vyama vyetu kusikiliza jinsi tunavyonadi sera zetu, na ahadi zetu na hatimaye siku ikifika wapige kura.
Kwa maana hiyo kulikuwa na utulivu nchi nzima, kwahiyo hapo sioni Chama Cha Mapinduzi kimelindwa vipi lakini kama nilivyosema mwanzo vyombo hivi ni vya taifa na vinawajibu kwa wananchi wake wote wakiwemo wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine.
Kikeke:Taarifa ya Tume imesema watu waliuawa kwa kupigwa risasi Oktoba 29 , kwanini mpaka sasa hakuna viongozi wa Serikali ya CCM ambao wamewajibika?
Dk.Migiro:Awali ya yote ninawajibu wa kusema Chama Cha Mapinduzi na Watanzania walio wengi taarifa za kifo zimetusikitisha sana , Jaji Chande alipokuwa anazungumza ametoa takwimu kuna watu takribani 518 ambao waliuawa.
Namba ambayo inatusononesha na alisema inaweza kuongezeka na walitupa vyanzo vyao kwamba kulikuwa na taarifa za hospitali binafsi ,hospitali za Serikali , Msajili wa Vizazi na Vifo ndio zilitoa namba hizi na wamesema inawezekana namba hii ikabadilika kwasababu wako ambao hawakwenda hospitali wala hawakwenda kusajili vifo.
Kikeke: Lakini Mheshimiwa Balozi swali langu lilikuwa kwanini hakuna mtu ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambaye amewajibika mpaka hivi sasa kwa yaliyotokea?
Dk.Migiro:Uwajibikaji ni suala muhimu sana na sisi Chama Cha Mapinduzi matumaini yetu yako kwenye tume ya uchunguzi wa jinai ambayo kazi yake itatoa mwanga zaidi katika suala la uwajibikaji ni muhimu .Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano alieleza wazi hakuna mtu aliyejuu ya sheria.
Kwa maana hiyo suala la uwajibikaji linanafasi kubwa sana ndani ya Chama Cha Mapinduzi na msisitizo huo tumeupata sio tu kwenye taarifa ya Tume na hata kwa kiongozi mkuu wa taifa letu .
Kama vipi tuwasiliane tupige stori
kuhusu majibu ya Dk.Migiro
0713833822

No comments:
Post a Comment