DKT. GHARIB BILAL AFUNGUA MKUTANO WA PAMOJA KATI YA TAASISI ZA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI ZA UWEKEZAJI MKOANI TABORA. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 19 July 2013

DKT. GHARIB BILAL AFUNGUA MKUTANO WA PAMOJA KATI YA TAASISI ZA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI ZA UWEKEZAJI MKOANI TABORA.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ddk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013 kwa ajili ya kufungua mkutano wa pamoja kati ya Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi, kuhusu uwekezaji mkoani Tabora. Mkutano huo umefanyika jijini Dar. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa (kulia) ni Julieth Kairuki.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akizindua Jarida maalum la Vivutio vya Uwekezaji vya mkoani Tabora, baada ya kufungua rasmi mkutano wa pamoja kati ya Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi, kuhusu uwekezaji mkoani Tabora, uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa (wa pili kulia) ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta na Julieth Kairuki. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua mkutano wa pamoja kati ya Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi, kuhusu uwekezaji mkoani Tabora, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kufungua mkutano huo.
 Julieth Kairuki, akizungumza.
 Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akiwahutubia kufungua mkutano huo.
 Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akiwahutubia kufungua mkutano huo.Kwa Picha zaidi bofya kwa hapa >>>

No comments:

Post a Comment