Matukio : Zuhura Maganga atwaa kwa kishindo nafasi ya Uenyekiti TAPSEA - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


16 May 2018

Matukio : Zuhura Maganga atwaa kwa kishindo nafasi ya Uenyekiti TAPSEAMwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga (katikati) akishangilia sambamba na wanachama wenzake wa TAPSEA baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguli wao uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar. Mwenyekiti huyo amepewa ridhaa hiyo ya kukiongoza chama hicho kwa mara nyingine tena baada ya muda wake wa awali kumalizika, ambapo alimshinda mpinzani wake, Habiba Mhina kwa zaidi ya asilimia 90.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), wakishangilia ushindi wa Mwenyekiti wao baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa Chama chao kwa mujibu wa Katiba yao.

Mjumbe Habiba Mhina aliyekuwa akiwania nafasi ya Uwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) akikijinadi ukumbini hapo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wao uliompa ushindi, Zuhura Maganga.

Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akiongoza kikao chake ya kwanza baada ya kutwaa kiti hicho kwa mara nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad