Viongozi wa ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza, ugeni
kutoka nchini Vietnam pamoja na wageni mbalimbali walioalikwa katika
sherehe hiyo wakigongesha vinywaji vyao ikiwa ni ishara ya kufurahi
kuwepo pamoja katika eneo hilo.
Rais wa Kiwanda cha Kutengeneza Kofia ngumu
za kisasa (Helmet) kilichopo nchini Vietnam, Greig Craft (kulia) akimpa
zawadi Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja (wa pili kutoka kulia) akitoa shukrani kwa ugeni kutoka nchini
Vietnam kwa kuitikia mwaliko wa kupata chakula cha jioni. Kulia ni Hoang
Thi Na Huong, Naibu Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu
(Helmet) kilichopo nchini Vietnam. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Jeshi
la Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna Edita Mallya. Anayefuata ni
Rais wa Kiwanda cha Kutengeneza kofia ngumu za kisasa nchini Vietnam,
Greig Craft, na wa katikati ni Gaston Sanga, Kamishna wa Utawala na
Fedha wa Magereza.
Wageni waalikwa wakishiriki chakula cha jioni pamoja
na Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja (katikati) akimtambulisha Gaston Sanga, Kamishna wa Utawala
na Fedha wa Magereza kwa ugeni kutoka nchini Vietnam. Wa pili kutoka
kushoto ni Deonice Chamulesile, Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa
Magereza. Ugeni huo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza wanatarajia
kujenga kiwanda cha kofia ngumu za kisasa (Helmet) nchini hivi karibuni
ili kuzuia ajali mbalimbali zinazotokana na pikipiki.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja akifurahia jambo na Rais wa Kiwanda cha Kutengeneza
kofia ngumu za kisasa nchini Vietnam, Greig Craft.
PICHA ZOTE
NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment