Balozi Mulamula akiwa na afisa wa Bunge Bw. Prosper Minja kabla ya kuanza kwa kiako cha Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama.Balozi Mulamula (kulia) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb) mjini Dodoma leo. Balozi Mulamula alifika Dodoma kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano wa sita wabunge ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma
Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Stephen Wasira ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu aliyemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula (kulia) akisalimiana na kubadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda Bungeni Dodoma leo.
Spika Makinda akifurahia jambo na Mbunge wa Simanjoro Mhe. Ole Sendeka (kati) na mdau wa michezo nchini,Wakili Imani Madega.
Balozi Mulamula (kulia) akisalimiana na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) leo katika viwanja vya Bunge Dodoma leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Hijra ya mjini Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma.
Picha na Aron Msigwa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment