Mkuu wa Mkoa DSM (kulia) Sadick Mecky apokea msaada wa waathirika wa mafuriko - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 16 January 2012

Mkuu wa Mkoa DSM (kulia) Sadick Mecky apokea msaada wa waathirika wa mafuriko

Mkuu wa Mkoa wa DSM Sadick Mecky Sadick (kulia) akipokea leo rasmi msaada kupitia kivuli kinachoonyesha vitu mbalimbali na thamani kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara wa kichina Tanzania ZHU JINFENG (katikati) kwaajili ya waathirika wa mafuriko jijini , Msaada huo umekabidhiwa jana kwa Makamu wa Rais Dkt, Gharib Bilal wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina wenye thamani ya shilingi milioni10. Pamoja na kukabidhi jan 15,2012 lakini leo wamewasilisha rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Meck Sadick jumla ya milioni 12.5 baada ya kuendelea kuchangia vitu vyengine vikiwemo mabati na saruji, (kushoto) Ni Mmoja wa ofisa kutoka chama cha wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang .
Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadick (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Fadhili Manongi (kushoto) leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM kwaajili ya waathirika wa mafuriko wa mkoa wa Da r es Salaam.
Mkuu wa Mkoa DSM (kulia) Sadick Mecky (katikati) Ofisa kutoka chama cha wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang pamoja na Katibu tawala wa Mkoa wa DSM Theresia Mmbando (kushoto) wakijadiliana leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM baada ya kukabidhi rasmi msaada huo wa kivuli cha mchango wenyethamani ya shilingi milioni 10 ambapo michango hiyo imeongezeka hadi kufikia 12.5/- (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

No comments:

Post a Comment