TACAIDS NA MASOKO AGENCIES WAANDAA WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WATANGAZAJI NA WAANDAJI WA VIPINDI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 4 November 2011

TACAIDS NA MASOKO AGENCIES WAANDAA WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WATANGAZAJI NA WAANDAJI WA VIPINDI

Afisa Uhusiano wa TACAIDS, Glory Mziray akielezea moja ya malengo ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandaaji wa vipindi na watangazaji wa redio za kijamii yaliyoanza jana jijini Mwanza, mafunzo hayo ni ya siku mbili, katika picha kulia ni mkurugenzi wa Masoko Agencies Yohana Mtweve.
Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza Goddfrey Mabu Chambuko akichangia mada katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watangazji na wandaaji wa vipindi vya redio za kijamii kutoka mikoa ya kanda ya ziwa.
Washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo wakimsikiliza mtoa mada kuhusu nguvu ya redio za kijamii Richard Ngaiza wa kampuni ya Masoko AGENCIES (T) LTD
washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo wakimsikiliza mtoa mada kuhusu nguvu ya redio za kijamii Richard Ngaiza wa kampuni ya Masoko AGENCIES (T) LTD
Mwanza
TUME ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imendaa mafunzo ya siku kuwajengea uwezo watangazaji,waandaaji na watayarishaji wa vipindi vya redio za kijamiii wa mikoa ya Kanda wa Ziwa, kupitia mtaalamu elekezi,Kampuni ya Masoko ANGENCIES (T) Ltd.
Mafunzo hayo yana lengo la kukuza uelewa kuhusu wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi (HIV/AIDS) kwa jamii, kuboresha vipindi vinavyohusiana na Ukimwi na kuharakisha na kuchochea zoezi la kubadili tabia katika jamii.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika jijini Mwanza yakishirikisha waandaaji wa vipindi na watangazaji wa redio za kijamii, wapatao zaidi ya 80 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Kagera,, Mara na Shinyanga.
Akitoa mada katika mafunzo hayo Afisa Uhusiano wa TACAIDS, Grory Mziray alisema mafunzo hayo kwa watangazaji na wanandaji wa vipindi yatawaezesha kuharakisha kampeni mbalimbali na malengo tarajiwa dhidi ya mapambano dhidi ya ukimwi kwa vile vituo hivyo vinasika zaidi katika jamii zinavizunguka.
“TACAIDS wameona vema kuandaa na mafunzo ya kuwajengea uwezo watangazaji na waandaaji wa vipindi vya redio za kijamii, kote nchini ili kukuza uelewa, afya kuhusiana na ukimwi na kuelimisha jamii ili iweze kubadili tabia kwa kutumia vipindi mbalimbali vitakavyoandaliwa na kutangazwa kupitia vituo vya redio hizo za kijamii” alisema Mziray.
Mbali na hilo waandaaji na watangazaji watafundishwa stadi za namna bora za kuandaa ama kutengeza vipindi bora vya ukimwi ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu,katika kuimareisha utendaji wazi wa TACAIDS.
Alisema redio hizo zitatumika kutoa taarifa sahihi kwa jamii ili iweze kuelewa athari za ukimwi na kufahamu umuhimu wa kupima ili kujua afya zao, na kuweza kujitambua na kujua namna ya kuishi kwa ambao wameambukizwa VVU.
Wananchi waishio katika maeneo mengi ya mjini wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa VVU kuliko vijijini , ingawa vijini wananwake wanathirika kuitokana na maumbile.
Changamoto nyingine ni kwa wanawake kujiingiza katika biashara ya ngono kwa ajili ya kipato, ngono kinyume cha maumbile na kuwa na wapenzi zaidi ya wawili, ambapo matumizi ya kondomu yako chini kwa kiwango cha wanawake 22 na wanaume 34 wanaoweza kutumia mipira kujikinga na mambukizi.
Mada mbili zilitolewa katika mafunzo hayo ambazo ni hali ya ukimwi nchini iliyotolewa na Grory Mziray wa TACAIDS na nguvu ya redio jamii katika kuleta mabadiliko ya maambukizi ya VVU iliyotolewa na Richard Ngaiza kutoka kampuni ya ANGENCIES (T) Ltd.
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watu waliombukizwa na wanaishi na VVU inafikia milioni 1.5 ambapo mkoa wa Ifringa ukiwa unaongoza Kwamba tatizo la kutopima ni moja ya changamoto kubwa zinazokabili jamii na TACAIDS katika udhibiti wa maambukizi mapya ya VVU.
Na Full shangwe blog

No comments:

Post a Comment