+255(0) 715 643 633 gadiola25@gmail.com
 • Mar 5, 2015

  Maisha Yetu : Rais Dk. Jakaya Kikwete Akutana na Viongozi wa Chama cha Albino Tanzania, Ikulu Dar


  Rais Kikwete akiongea  na ​Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015  alipowakaribisha  ili kusikiliza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​

  Soma Habari Kamili Hapa.....
  No comments

  Matukio :Mnuso wa Bloggers Watikisa Jiji la Dar, MCT watambua Mchango wa Blogs Tanzania


  Kutoka Kushoto; ni Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog, Sufiani Mafoto wa Sfianimafoto.com , Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog (Arusha) na Josephat Lukaza wa Josephatlukaza.com Wakisubiria Keki kwa Hamu , katika Mnuso wa Tanzania Bloggers Network iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar  es Salaam.
  Mgeni rasmi katika Mnuso wa bloggers ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akitoa mawili matatu kwa bloggers na kuahidi kuwa kuanzia mwaka huu bloggers wataingia katika tuzo mbalimbali zinazoendeshwa na MCT 
   Mrs Jeff (kushoto) akiwa na Mrs Ankal (katikati) na Shamim Mwasha wa 8020 fashion blog wakati wa mnuso wa bloggers
   Gadiola Emanuel kutoka Wazalendo 25 Blog Arusha(Kulia) akiwa na Ankal (Katikati) na Zainul Mzige kutoka dewji blog
   Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akisalimiana na Mmiliki wa Lukaza Blog, Josephat Lukaza wakati wa mnuso wa wamiliki wa Blog uliofanyika usiku wa Kuamkia Jana katika Hoteli ya Serena. Wanaoshuhudia pembeni Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Joachim Mushi na Mmiliki wa Michuzi Blog, Issa Michuzi
   Mgeni rasmi katika Mnuso wa Bloggers ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) akijadiliana jambo na Adela Kavishe ambae ni Mmoja kati ya wamiliki wa blog hapa Tanzania, Katikati ni Monica Joseph
   Baadhi ya Bloggers wakiwa katika picha ya Pamoja
   Cheers
   Khadija Kalili akisalimiana na Mgeni rasmi ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga wakati wa mnuso
   Mwenyekiti wa muda wa Mtandao wa Wamiliki wa Blog Tanzania (Tanzania Bloggers Network) Joachim Mushi akimkaribisha Mgeni rasmi kwaajili ya kutoa maneno mawili matatu kwa wamiliki wa blog.
   Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa akiongea jambo mbele ya Wanablog na wageni rasmi juu ya udhamini mkuu walioutoa katika mnuso huo kwa kutambua mchango wa blogs Tanzania
   Burudani kutoka kwa Jhikoman
   Mgeni rasmi akikata ndafu 
  Mwakilishi wa Bloggers Rahel Pallangyo akilishwa ndafu na mgeni rasmi Katika Mnuso huo
   Adela Kavishe na Mdau Faustine Ruta wa Bukoba wadau Blog wakiwa mbele ya Ucanon wa Lukaza Blog
   Serebuka Serebuka unaweza pendwa tena........
   Faustine Ruta wa bukoba wadau blog katika ucanon wa Lukaza Blog na Josephat Lukaza
   Makala na Woinde kwa pamoja
   Monica Joseph na Mkurugenzi wa Masoko Wa Vodacom Kelvin Twisa
  Ankal akiwa na Faustine Ruta na Crant wakati wa mnuso wa bloggers.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
  No comments

  Matukio : Baraza la Ushauri SUMATRA Lazindua Vilabu vya Wanafunzi ,Jijini Dar es Salaam


   Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Ayoob Omary akizindua vilabu vya wanafunzi vya Sumatra. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo na kulia ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatan.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
   Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza.
   wanafunzi wakifuatilia hotuba za uzinduzi kutoka kwa viongozi.
   Mgeni rasmi pamoja na meza Kuu ikipiga picha na Vilabu mbalimbali kutoka shule za sekondari na msingi.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay, Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi wa klabu za wanafunzi watumiaji wa huduma za usafiri mkoa wa Dar es salaam jana. Wengine ni  Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano na Mwenyekiti wa Baraza hilo Ayoob Omary. Picha na Stori: mrokim.blogspot.com
  No comments

  Afya Zetu : Wananchi watakiwa kujitokeza kwenye kambi ya Kupima Afya Bila malipo kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka 5


  DSCN9331 DSCN9215
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk Ali Mzige (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Kambi ya kupima afya bila malipo kwa watoto wadogo, itakayofanyika Jumapili ya Machi 8 mwaka huu. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy na kulia ni mwakilishi wa shule ya Kibugumu, Mwalimu Mzamili Ally.
  Na Andrew Chale modewji blog
  Imeelezwa kuwa, Sensa ya mwaka 2012 ilionesha kuwa asilimia 42 ya watoto chini ya miaka 5 hapa Nchini Wamedumaa, asilimia 16 wana uzito pungufu (wako underweight), asilimia 5 wamekonda (marasmic) wako kwenye kadi nyekundu ya mtoto.
  Hayo yamesemwa jana Machi 4, jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk Ali Mzige mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa juu ya kambi ya upimaji wa afya kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 5, itakayofanyika Jumapili ya Machi 8, katika shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, wilaya ya Temeke.
  Dk. Mzige alibainisha kuwa kama ilivyo kwa watu wazima, upimaji wa afya ya watoto wenye umri chini ya miaka 5 una manufaa makubwa kwa mtoto, familia na jamii ya watanzania wote.
  Ambapo alibainisha kuwa, tatizo la utapia mlo kwa watoto hapa nchini imepelekea Tanzania kuwa nafasi ya tatu katika Bara la Afrika, Lishe duni kwa watoto na wajawazito huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ikiongoza na Ethiopia ikiwa ni ya pili kwa tatizo hilo la utapiamlo.
  DSCN9217
  Hata hivyo Dk. Mzige alibainisha kuwa, utapiamlo huo unaonekana nchini upo kwenye mikoa inayozalisha chakula na matunda kwa wingi ikiwemo ya Morogoro, Mbeya, Tanga, Rukwa, Iringa na Manyara.
  Pia alieleza kuwa tatizo lingine ni la utapiamlo la kula chakula kupita kiasi kama vyakula vyenye wanga na sukari kwa wingi, mafuta kwa wingi na kuleta maradhi/magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watoto na watu wazima.
  Aidha, Dk. Mzige alisema kuwa elimu sahihi dhidi ya kupambana na maradhi hayo ya utapiamlo, yatatolewa kwenye kambi hiyo huku akisisitiza wazazi kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani itakuwa ni ya kipekee na faida kwao na kwa watoto wao.
  “Tujitokeze kupima afya zetu na pia watoto hasa wadogo. Hivyo kambi hii itakuwa msaada mkubwa kwani tutachunguza yale magonjwa mengi yanayowakabili watoto wengi hapa nchini.” Alisema Dk. Mzige.
  DSCN9242
  Dk. Mzige akionyesha mswaki wa mti ambai ni wa asili, ambapo alishahuri watanzania kuwa na tabia ya kubadilisha miswaki yao kila baada ya miezi mitatu, ama kutumia miswaki ya miti ambayo inasaidia kuboresha meno.
  Akitoa baadhi ya takwimu zinazowakabili watoto wengi hapa nchini, ni pamoja na :
  Watoto 130, walio chini ya umri wa miaka 5 hufa kila siku hapa Nchini kwa ajili ya utapiamlo (Malnutrition-Lishe duni).
  Upungufu wa wekundu wa damu asilimia 59 kwa watoto wenye miezi 6 hadi 59. Asilimia 33 ya watoto chini ya miaka 6 wana ukosefu wa vitamin A.
  BANGO SANGHO, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy alisema kuwa kwa kushirikiana na Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), ya Jijini Dar es Salaam ambapo wameandaa kambi hiyo ya kupima afya bila malipo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ni faraja kwa jamii hiyo kwani watoto wengi hapa Nchini wamesahulika katika kupimwa afya zao.
  DSCN9265
  Dk. Mzige akionesha Yai ambapo alibainisha kuwa Yai sio zuri kwani lina Cholesterol hivyo mtu anashahuriwa kula mayai matatu kwa wiki hasa ya kuchemsha.
  Amit Nandy aliwataka wananchi wa Kigamboni na maeneo mbalimbali kuwapeleka watoto wao katika shule ya Msingi, Kibugumu kwa ajili ya kupimwa afya zao hizo ikiwemo magonjwa yanayowakabili watoto wengi.
  “wazazi wote tunawaomba kujitokeza kwa wingi, Machi 8, katika shule ya Msingi Kibugumu mukiwa na watoto wenu pamoja na makadi ya kliniki ilikuweza kupata huduma ya matibabu bure.
  Madaktari bingwa na matabibu watapima magonjwa mbalimbali ikiwemo Afya ya kinywa, Uzito, Ukaguzi na ushauri wa lishe. Pia watakaobainika kuwa na matatizo maalum ya kiafya watapewa rufaa” alieleza Amit Nandy.
  Ambapo alibainisha kuwa, huduma hizo za matibabu zinatarajiwa kutolewa kuanzia asubuhi ya saa tatu hadi saa saba mchana. (Saa 3:30 asubuhi-Saa 7-30 mchana).
  DSCN9264
  Dk Mzige akionyesha soseji ambapo alisema kuwa ulaji wa soseji sio mzuri kwa afya hivyo watu wanatakiwa kuepuka ama kupunguza.
  DSCN9252
  Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo.
  No comments

  Teknolojia Yetu : DK. Jakaya Kikwete Kuzindua Studio za Azam TV , Bilioni 56 zatumika Kujenga


  JUMLA dola za Kimarekani Milioni 31 (zaidi ya Sh. Bilioni 56 za Tanzania) zimetumika kutengeneza studio mpya za kisasa za Azam TV, zilizopo eneo la Tabata Relini, Dar es Salaam.Hayo yamesemwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando wamiliki wa Azam TV leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Tabata, Dar es Salaam. Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza kampuni kubwa za vyombo vya habari zikiwemo Idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Mwananchi Communication Limited (MCL), amesema studio hizo zina ubora kuliko nyingine zote nchini. Kwa Maelezo Zaidi Bofya Hapa >>>
  No comments

  Jamii Zetu : Dk. Gharib Bilal Afungua Mkutano wa Pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamishina Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, wakati walipokutana baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Burn Ltd, Malaczynski Burn, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia alipokuwa akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015. Picha na OMR.
  No comments

  Jamii Zetu : UN Yazindua ripoti ya Dawa za Kulevya Duniani


  Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa ripoti ya Kupambana na dawa za kulevya ya Umoja wa Mataifa. Kulia ni mgeni rasmi Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi na kushoto ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama.

  Na Andrew Chale wa Modewji blog.

  Uongozi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataaifa (UNIC) umezindua ripoti ya Kupambana na dawa za kulevyaa ya Umoja wa Mataaifa, Uzinduzi uliofanywa Machi 4, Jijini Dar es Salaam.

  Wakizungumza mbele ya wandishi wa habari kwa upande wake, Afisa Habari wa Kituo Cha Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alibainisha ripoti hiyo imeweza kuchambua mambo mbalimbali dhidi ya dawa za kulevya na mikakati iliyofikiwa.

  Ambapo alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na kupungua kwa wimbi la kuingia kwa dawa za kulevyaa nchini hasa kupitia njia za bahari ya Hindi huku mji wa Mexico wa America, ukipunguza kwa asilimia kubwa matumizi ya dawa za kulevya.

  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Komputa wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi akizindua kitabu cha ripoti ya Bodi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Umoja wa Mataifa, kwenye hafla ya uzinduzi uliofanyika Machi 4, MAELEZO, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Mipango wa Umoja wa Mataifa, Immaculata Malyamkono-Nyoni na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupambana na Watumiaji wa Madawa ya Kulevya,Very Kunambi. (Picha na Andrew Chale).

  Vuzo alibainisha kuwa, pia mikakati iliyofikiwa ambayo pia imo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mfumo wa kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya wanaoacha kwa kuwapatia dawa maalum za kupunguza taratibu matumizi hayo.

  ‘Mipango ya kuwapatia wale wanaocha dawa maalum za kusaidia utumiaji wa madawa na pia dhidi ya kupambana na dawa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi wa watumiaji” alisema Vuzo.

  Aidha, alibainisha kuwa,  Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine .

   Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi akionyesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

  Kwa upande wake  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya kudhibiti  Ukimwi DCC, January Ntisi ,amesema wanashirikiana katika kupambana na dawa za kulevya na umoja huo kwani Tanzania ni miongoni nchi ambazo pia zinakabiriwa na tatizo hilo.

  Alisema mwaka jana walikamata dawa tani 2.3 ambazo zingeingia nchini kungekuwa na kundi kubwa ambao wanatumia dawa hizo.

  Kwa upande wake, Immaculate Nyoni ambaye ni Project officer UNODC alibainisha juhudi mbalimbali zinafanywa katika kukabiliana na wimbi la dawa za kulevya duniani kote ambapo kwa sasa angalau matumizi hayo yakiendelea kupungua.

  Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti  Ukimwi (DCC), January Ntisi akifafanua jambo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.

  Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa kupambana utumiaji wa Madawa ya Kulevya waliohudhuria uzinduzi huo.

  No comments

  Matukio na Habari :Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ahimiza watumishi wake kuendelea kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha kawaida ambacho ufanyika kila baada ya miezi mitatuKikao hicho kimefanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Magreth Mtaki.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel akafafanua jambo wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Magreth Mtaki.
  Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bibi. Magreth Mtaki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakifuatilia mada kuhusu bajeti ya Wizara iliyowasilishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo Mwanzala Kayoka (hayupo pichani).
  Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Mwanzala Kayoka akiwasilisha mada kuhussu uelekeo wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 na 2015/16 wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na watumishi wote kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Liwa akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na watumishi wote kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Bib. Beatrice Sumari akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kawaida baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na watumishi wote kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM.
  No comments

  Tokomeza Ebola Duniani


  KARIBU KATIKA BLOG YA WAZALENDO 25 BLOG.TUTUMIE HABARI NA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI. TUNAKARIBISHA WADHAMINI NA MATANGAZO YA BIASHARA. KWA UDHAMINI NA MATANGAZO WASILIANA NASI KWA NAMBA 0715 643 633. Email: gadiola25@gmail.com .WELCOME TO WAZALENDO 25 BLOG, SEND US PHOTO EVENTS, NEWS AND ADVERTISEMENT.CONTACT US THROUGH 0755 643 633. Email: gadiola25@gmail.com

  Tokomeza Ukeketaji kwa Watoto wa Kike