Matukio : Hafla ya Kukabidhi hati za Utambulisho za Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 9 June 2018

Matukio : Hafla ya Kukabidhi hati za Utambulisho za Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria





Tarehe 7 Juni 2018 kuanzia saa 5:30 hadi 6:15 Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidini Ally Mboweto, alikabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria Mhe. Muhammadu Buhari. Hafla hiyo ilifanyika katika Ikulu ya nchi hiyo Jijini Abuja na kuhudhuriwa na Mke wa Mhe. Balozi, Hajat Ashura Ally Mboweto, Maafisa wa Ubalozi na viongozi mbalimbali wa serikali ya Nigeria. Yafuatayo ni matukio katika picha wakati wa hafla hiyo;-

Mhe. Balozi Mboweto akiwasili Ikulu na kupokelewa na Mkuu wa Itifaki wa Ikulu

Mhe. Balozi Mboweto akielekea kwenye uwanja wa gwaride.

Mhe. Balozi akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wa jeshi la Nigeria.




Mhe. Balozi akikagua gwaride
Mhe. Balozi akielekea kwenye ukumbi wa Ikulu baada ya kukagua gwaride.

Mhe. Rais Buhari akiwa na Waziri wa nchi (Mambo ya Nje) na Katibu wa Rais akimsubiri Mhe. Balozi.


Mhe. Balozi akikabidhi Hati kwa Mhe Rais Buhari







Mhe. Balozi akisalimiana na Mhe. Rais Buhari baada ya kukabidhi Hati.




Mke wa Mhe. Balozi, Maafisa Ubalozi na viongozi mbalimbali wa serikali ya Nigeria wakishudia tukio la kukabidhi Hati.

Mhe. Balozi akiwa katika mazungumzo ya falagha na Mhe. Rais Buhari.




Mhe. Balozi akitambulishwa kwa viongozi wa jeshi la Nigeria.







Mhe. Balozi akisaini kitabu cha wageni Ikulu akishuhudiwa na mkewe pamoja na Maafisa Ubalozi.

Mhe. Balozi akiagana na Mkuu wa Itifaki Ikulu baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi Hati.



Mhe. Balozi akiondoka Ikulu

No comments:

Post a Comment