Matukio : Kamishna Jenerali wa Magereza Awavisha vyeo Maofisa Waandamizi Tisa wa Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Jun 2018

Matukio : Kamishna Jenerali wa Magereza Awavisha vyeo Maofisa Waandamizi Tisa wa Jeshi la Magereza Jijini Dar es SalaamKamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo akimvalisha cheo Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila kuwa Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga kuwa Naibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.

Makamishina na Manaibu Kamishna wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2018.Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.

Baadhi ya Maafisa Wastaafu na waliopo sasa wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hafla fupi ya uvishaji vyeo kama inavyoonekana katika picha.

amishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliowavalisha vyeo hivyo kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli ambapo hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 8, 2018.Picha zote na Jeshi la Magereza


KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli amewavisha vyeo maafisa wa ngazi ya juu 9 wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Miongoni mwa maafisa 9 waliovishwa vyeo ni manaibu kamishna wa magereza – DCP wanne wa Jeshi hilo ambao wamepandishwa vyeo na kuwa Makamishna wa magereza, huku makamishna wasaidizi waandamizi wa Magereza -SACP watano wakipandishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna – DCP wa Jeshi hilo.


Waliovishwa vyeo kuwa Makamishna wa Magereza ni Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Naibu Kamishna wa Magereza Gideon Nkana ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam.


Wengine waliovishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Julius Sang’udi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Phaustine Kasike, Mkuu wa Kitengo cha Parole pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Jeremiah Katungu ambaye ni Katibu Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza.


Akizungumza mara baada ya kuwavisha vyeo Maafisa hao wa magereza(Ijumaa, Juni 8, 2018) katika hafla ya kuwavisha vyeo hivyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa amewataka makamishna hao wa Jeshi la magereza wa ngazi zote kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu sambamba na kusimamia haki na usawa katika utekelezaji wa majukumu yao kila siku.


Aidha, Jenerali Malewa amemshukru Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli kwa kuwapandishwa vyeo maafisa hao ambao watajaza nafasi mbalimbali za juu za uongozi ndani ya Jeshi la Magereza kwani kwa muda mrefu safu ya juu ya uongozi ilikuwa na upungufu mkubwa wa kada ya maafisa wa vyeo hivyo hali iliyopelekea kuathiri utendaji kazi wa Jeshi hilo.


Maafisa hao kabla ya kuvishwa vyeo hivyo walivyotunukiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia Juni 02, 2018, walipata fursa ya kula kiapo cha Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya katibu wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad