Afya : Waziri Ummy Mwalimu Azindua Benki ya Damu Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday 3 November 2017

Afya : Waziri Ummy Mwalimu Azindua Benki ya Damu Jijini Dar es Salaam






Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.

Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam , katikati waliokaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Lwezimula.

Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem kulia akimkabidhi zawadi ya mchango mkubwa katika Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu kushoto wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam.


Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.

Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem akichangia damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Lwezimula aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam, kulia aliyekaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakimsikiliza kwa makini ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam.

Mwanachama wa Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa Wanawake (WOW) Afrika Mashariki Bi. Rehema Mwangolombe akiwa katika maandalizi ya kuchangia damu damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA ALLY DAUD- WAMJW

No comments:

Post a Comment