Uwekezaji : TADB Yang'arisha Kongamano la Biashara na Uwekezaji, China - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Oct 2017

Uwekezaji : TADB Yang'arisha Kongamano la Biashara na Uwekezaji, China



Pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwana FRANCIS Assenga akiwa kwenye Kongamano la Biashara, Viwanda na Uwekezaji kati ya Tanzania na China lililofanyika katoka Hoteli ya Shangrila Jijini Guanzhou, China mwishoni mwa wiki, ambapo pamoja na mambo mengine TADB iliweza kutangaza huduma zake na jinsi fursa mbali mbali za kuvutia wawekezaji toka China na Ubia kwenye miradi mbali mbali ya Kilimo nchini Tanzania ikiwemo miundo mbinu ya Umwagiliaji; Maghala ya Kisasa na Masoko.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga kushoto akimkabidhi zawadi ya Benki Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ua Afrika wa China (CADFUND) anayeshughulikia Viwanda, Kilimo, Afya na Uwekezaji Bwana Lei Ma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda na Kulia ni Makamu Rais na Naibu Mtendaji Mkuu wa 'CADFUND' Bwana Wang Yong mara baada ya kumalizika kwa Kikao baina yao mjini Guangzhou juzi.

Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Makamu Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China 'CADFUND". Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga, Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Bw. Adolf Nkenda, Makamu Rais na Naibu Mtendaji Mkuu wa CADFUND, Bw. Wang Yong na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja.



Na Saidi Mkabakuli


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeng'arisha Kongamano la Biashara, Viwanda na Uwekezaji lililofanyika Jijini Guangzhou nchini China mwishoni mwa wiki; ambapo Viongozi wa Serikali, Sekta Binafsi na Wafanyabiashara zaidi ya 80 toka Tanzania walihudhuria na kupata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo ya uwekezaji na biashara na wenzao wa China.

Aidha, Benki ya Kilimo Tanzania iliweza kujadiliana na wadau mbali mbali wa kilimo kwenye mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya kilimo ambapo wengi walionesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania.

Katika Kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Killimo Tanzania Bw. Francis Assenga aliweza kuwa na mazungumzo ya kina na Mkurugenzi wa Shirika la Serikali ya China la Sinolight Holdings Corporation linalojishughulisha na Uagizaji wa Mihogo toka nchi mbali mbali duniani Bwana Du Chuan ambako pamoja na masuala ya uwekezaji kwenye zao la mihogo nchini, walijadiliana pia fursa zilizopo China kwa Watanzania kwenye kilimo cha mihogo, hususan kwenye kuongeza thamani ya zao hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad