Afya Zetu: Naibu Waziri, Dk. Ndungulile afanya kujiridhisha na hali ya Upatikanaji wa Dawa - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 17 October 2017

Afya Zetu: Naibu Waziri, Dk. Ndungulile afanya kujiridhisha na hali ya Upatikanaji wa Dawa



Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Mwananyamala Bw. Marco Sallingu kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya ,jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa pili kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za wa Hospitali ya Mwananyamala wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya, jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD kutoka kwa Mfamasia wa Hospitali ya Sinza Palestina Bi. Doris Messanga kulia wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya  jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa katikati waliosimama akiongea na wagonjwa wakati wa ziara yake Hospitalini Sinza Palestina alipotembelea vituo vinavyotoa huduma ya afya jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa tatu kulia akiangalia nyaraka zinazoonesha jinsi ya dawa zinavyoagizwa MSD katika Zahanati ya Mwenge wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya, jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile wa kwanza kulia akiangalia dawa ziliozopo katika stoo za Zahanati ya Mwenge wakati wa ziara yake katika vituo vinavyotoa huduma ya afya , jijini Dar es salaam.

…………………

NA WAMJW-DAR ES SALAAM


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amefanya ziara kwenye baadhi ya vituo vitoavyo huduma za afya kwa ajili ya kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa jijini Dar es salaam.


Akizungumza lengo la ziara hiyo Dkt. Ndungulile amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuungana na Mhe. Rais wa wamau ya tano Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kutatua tatizo la dawa katika vituo vinavyotoa huduma za afya mpaka kufikia 2020.


“Mpaka kufikia hivi sasa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga shilingi Bilioni 262 kwa ajili ya kutatua tatizo la uhaba wa dawa nchini kutoka shilingi bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/2016 “ alifafanua Dkt. Ndungulile.


Aidha Dkt. Ndungulile amesema kuwa katika ziara hiyo amegundua kwamba vituo vinavyotoa huduma ya afya vina dawa zote muhimu isipokuwa kuna upungufu wa vifaa tiba ambapo tatizo hilo litafanyiwa kazi mara moja .


Mbali na hayo Dkt. Ndungulile aliwataka waganga wakuu na Wafamasia wa vituo vinavyotoa huduma za Afya kuboresha upokeaji ,utunzaji wa dawa pindi zinapoingia kwenye stoo zao na usimamizi mzuri wa dawa hizo.


“Vituo vinavyotoa huduma za afya lazima ziwe na kamati za afya ambazo zitashiriki katika kupokea dawa pindi zinapotoka MSD badala yake zinapokelewa na mtu mmoja aidha mfamasia au mtumishi mwingine wa kitengo cha dawa” alisema Dkt. Ndungulile.


Dkt. Ndungulile, amefanya ziara yake ya kutaka kujiridhisha na hali ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mwananyamala,Hospitali ya Sinza na Zahanati ya Mwenge za jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment