Utalii wa Ndani : Kamati ya Kudumu ya Bunge yatembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami,Morogoro - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 5 September 2017

demo-image

Utalii wa Ndani : Kamati ya Kudumu ya Bunge yatembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami,Morogoro





DSC_1703
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya kikazi katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki/Ushoroba mkoani Morogoro ambayo iliyolenga kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
DSC_1700
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakimsikiliza Afisa Wanyamapori Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Leonard Mayeta (wa nne kulia) wakati akitoa maelezo kuhusu Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki/Ushoroba wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye hifadhi hiyo ambayo ililenga kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
DSC_1825
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Utalii wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi akiwasilisha taarifa ya mamlaka hiyo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. James Wakibara mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada ya kutembelea eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki mkoani Morogoro.
DSC_1708
DSC_1750
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia) wakiongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kupanda mlima katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro wakati wa ziara yao iliyolenga kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
DSC_1784
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya kikazi katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani.
DSC_1791
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru, Cathbert Mafupa (kushoto) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu Hifadhi hiyo.
DSC_1796
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mary Chatanda (wa tatu kushoto) akizungumza kutaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo kuhusu Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru wakati wa ziara ya kamati kwenye hifadhi hiyo. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa nne kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo (wa pili kulia).
DSC_1804
DSC_1773
Wajumbe wa Kamati wakikagua eneo la Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro wakati wa ziara yao ya kikazi ya kuangalia changamoto mbalimbali za uhifadhi zinazoikabili hifadhi hiyo kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
DSC_1806
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akiongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru.
DSC_1807
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na Wajumbe wa Kamati hiyo wakitembelea eneo la Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru.
DSC_1760
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko (kulia) ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo kwenye ziara hiyo.
DSC_1829
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akiwasilisha taarifa ya taasisi hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada ya kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro jana wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyolenda kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
DSC_1830Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akiwasilisha taarifa ya taasisi hiyo mbele ya Kamati.
DSC_1776
DSC_1761
PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA-WIZARA YA MALIASILI

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *