Jeshi : Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Wahitimu Mafunzo ya JKT - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 5 September 2017

demo-image

Jeshi : Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Wahitimu Mafunzo ya JKT


719A4167
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa wamejipanga kusubiri sherehe za mahafali ya kumaliza mafunzo ya JKT kuanza. Mafunzo hayo yalifanyika Kambi ya JKT ya Oljoro mkoani Arusha kwa kipindi cha wiki sita kuanzia tarehe 24 Julai hadi 04 Septemba 2017. 719A4196
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa mahafali hayo akiwa katika jukwaa kwa ajili ya kupokea heshima kutoka kikosi cha Vijana cha Operesheni Viwanda (hakipo pichani) ambacho kimejumuisha watumishi 30 wa Wizara ya Mambo ya Nje. 719A4213
Mgeni Rasmi, Balozi Mlima akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshima yake na kikosi kilichohitimu mafunzo ya JKT ambacho kilijumuisha watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje719A4313
Mgeni Rasmi, Balozi Aziz Mlima wakiwa wamesimama pamoja na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (kulia) na Kamanda wa Kambi ya Oljoro kwa ajili kuangalia vikosi vikipita mbele yao katika mwendo wa pole na kasi719A4276
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole
719A4372
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa kasi
719A4443
Mgeni Rasmi akikabidhi zawadi kwa waliofanya vizuri zaidi.
719A4447
Bi. Khadija Othman akipokea zawadi yake
719A4456
Bw. Graison Ishengoma akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni Rasmi
719A4463
Bw. Edward Komba akipokea zawadi yake. 719A4486
Wahitimu wa mafunzo ya JKT kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakila kiapo cha utii
719A4514
Risala kwa Mgeni Rasmi. katika risala hiyo waliahidi kuyafanyia kazi mafunzo yote waliyoyapata watakaporejea katika kituo chao cha kazi. Walijifunza uzalendo, utii, ustahamilivu, ukakamavu na mengine mengi.
719A4549
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao nao washapitia mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wakiwashuhudia wenzao wakihitimu mafunzo ya JKT katika awamu ya pili.
719A4567
Burdani ilikuwepo siku ya mahafali. Hapo bendi ya Jeshi ikitumbwiza.
719A4656
Onesho la Makamandoo hapo mmoja wao amebeba ndoo za maji kwa kutumia meno yake.
719A4683
Mkuu wa Kambi ya Oljoro akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkuu wa JKT ili amkaribishe Mgeni Rasmi
719A4706
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT akimkaribisha Mgeni Rasmi atoe hotuba ya kufunga mafunzo hayo. Kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi alisisitiza umuhimu wa taasisi nyingine za umma kuiga Wizara ya Mambo ya Nje kwa kupeleka watumishi wao ili kupata mafunzo ya JKT ambayo ni muhimu kwa kujenga uzalendo, nidhamu na umoja.
719A4714
Mgeni Rasmi akisoma hotuba yake. Alitoa ushuhuda kuwa watumishi walioshiriki mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wameonesha umahiri mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na ndio sababu amepeleka kundi lingine katika awamu ya pili. Aliahidi atawapeleka watumishi wa Wizara yake wenye sifa ikiwemo ya umri (chini ya miaka 40) hatua kwa hatua hadi watakapomalizika.
719A4729
Wahitimu wa mafunzo ya JKT wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi719A4686
Baadhi ya wageni waliohudhuria mahafali hayo. Hapo afande anateta na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Bw. Othman Rashid.
719A4788
Mkurugenzi wa Utawala katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nigel Msangi akimpongeza Bw. Wambura kwa kuhitimu mafunzo ya JKT. 719A4810
Tumemaliza salama, shukran kwa Wizara kwa kutuandalia mafunzo haya yenye tija kubwa kwetu.


719A4797
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala; Bi. Ngusekela Nyerere na Mwalimu wa somo la Uzalendo ambaye alikuwa Msadizi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
719A4806
Furaha tumemaliza mafunzo, Kutoka kushoto ni Felista Rugambwa, Teodos Komba na Rose Mbilinyi.
719A4842
Wakiwa katika pose baada ya kumaliza mafunzo.
719A4900
Wanaimba nyimbo za jeshi. 719A4748
Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi na wahitimu wa JKT.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *