Burudani : BASATA Yanogesha Raha za Pwani Nchini Marekani - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


21 Jul 2017

Burudani : BASATA Yanogesha Raha za Pwani Nchini MarekaniBASATA YANOGESHA RAHA ZA PWANI NCHNI MAREKANI:

Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza linalo simamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) - Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA, akifuatana na Msanii maarufu wa nyimbo na ngoma ya Muduara- Bwana ALI RAMADHAN ALI, al-maarufu kwa jina la MR. AT, wamewasili kwenye Uwanja mkuu wa ndege wa Dulles Internatinal Airport (IAD) mjini Washington, DC, jana Alhamisi, 20 Julai, kwa ajili ya kushiriki katika jopo au Kongamano la RAHA ZA PWANI, lenye lengo la ku utangaza na kudumisha Utamaduni wa Mswahili na Lugha yake adhim.

Tamasha hilo ambalo hutayarishwa na kampuni ya Swahili Media Network, litafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 22 Julai, kwenye ukumbi wa the Hampton Inn, 9670 Baltimore Avenue, College Park, MD, kuanzia saa 10:00 jioni hadi Saa 5: 00 Usiku.

Wageni wengi kutoka maeneo ya DMV wamekaribishwa, ili kijifunza, kusherehekea na kufurahia vionjo vya Pwani, Mitindo ya Mavazi, Sanaa za Kiswahili na Dansi Laivu.

Hii ni Mara yao ya kwanza kwa wajumbe hawa wa Bongo kuingia Marekani.

Walipokelewa kwa furaha na wenyeji wao pamoja na Wadau wenye kufuatilia na kuupenda Utamaduni wa PWANI na Sanaa zake mbali mbali.

Kabla ya kurejea Tanzania, wajumbe hawa wanatatajia kuitembelea miji mingine kadhaa ya Marekani pamoja na taasisi zinazo husika na Sanaa na Utamaduni.

Post Top Ad