Michezo: Simba Day Kuzinduliwa Agosti 30 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Monday, 25 August 2025

Michezo: Simba Day Kuzinduliwa Agosti 30

 


"Katika msimu huu wa 17 wa Simba Day, utazinduliwa rasmi Agosti 30, 2025, na kama ambavyo tumeanzisha utamaduni wa kufanya uzinduzi wa Wiki ya Simba nje ya jiji la Dar es Salaam basi na mwaka huu itakuwa hivyo. Mwaka jana ilikuwa Morogoro na mwaka huu tutazindua mkoani Iringa kwenye wilaya ya Mafinga. Tutaondoka Dar tarehe 30/08/2025 na uzinduzi rasmi utafanyika Agosti 31, 2025 kwenye viwanja vya Mafinga vilivyopo Mafinga Mjini."


"Awali tulipanga iwe Iringa Mjini lakini baada ya maoni na majadiliano tukaona tuhamishie Iringa, nichukue nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wa Iringa Mjini. Niwaombe sasa Wanasimba wote wa iringa na Wanasimba wote wa Nyanda za Juu tukutane Mafinga kwa uzinduzi wa Wiki ya Simba. Uzinduzi ambao tutaufanya Mafinga haijawahi kutokea. Kwanza kwa wingi wa watu, pili kwa ukubwa wa tukio na tatu kwa shamrashamra ambazo zitafanyika. Nichukue nafasi kuwakaribisha wote ambao wangependa kushirikiana nasi."- Semaji Ahmed Ally.

"Septemba 3, 2025 kutakuwa na droo ya bonanza. Mwaka jana mmnakumbuka tulikuwa na bonanza lilishirikisha matawi. Na mwaka huu tutarudisha tena na linahusisha matawi yote ya Simba Sports Club. Matawi yote ambayo yanataka kushiriki tutawapa namba ya kutuma jina lenu kushiriki. Tunafanya hivi ili kutengeneza umoja na upendo kwenye matawi ya Simba. Na hapa sio matawi tu ya Dar es Salaam hata matawi ya mikoani."


"Mwaka jana tuliwaalika Simba Legends walipiga mpira mkubwa kwelikweli, kina Haruna Moshi, kina Banka. Mwaka huu kutakuwa pia na mechi ya wanawake na ili kunogesha zaidi kutakuwa na mechi ya vibonge, nikisema vibonge namaanisha vibonge kwelikweli. Chico ndio kocha wa hiyo timu."


"Septemba 4, 2025 ni siku ya matawi, tunafahamu yapo matawi mengi wanahitaji kuzinduliwa matawi yao. Tayari tuna matawi mawili hapa na kama kuna mwingine amekamilisha utaratibu wote awasiliane na mkurugenzi wa Wanachama wa Simba."- Semaji Ahmed Ally.

"Simba ina watu wengi ambao wamefanya makubwa na kwenye Simba Day huwa ni siku sahihi ya kuwatunza. Mwaka huu kwenye Simba Day tutawaalika na kuwatunza wachezaji wa zamani ambao wamefanya makubwa na tutawapa tuzo ya heshima, wachezaji hawa ni John Bocco lakini vile vile tutakwenda kumuaga nahodha wetu mwingine ambaye ameitumikia Simba SC kwa miaka 15, Jonas Gerald Mkude na tutaendelea kuwaaga malengendari wetu taratibu taratibu tutakapopata nafasi. Mnayemsubiri tutamuaga akishamaliza kuchukua pension yake."


"Kikosi chetu kinatarajia kurejea nchini Agosti 28, 2025 siku ya Alhamisi lakini pia kikiwa nchini Misri kitacheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea nchini. Timu ambayo tutacheza nayo Simba Day tutaitangaza baadae."- Semaji Ahmed Ally.

No comments:

Post a Comment