Matukio : Kijiji cha Shujaaz Chafunguliwa katika Mashindano ya EAC 2017 Mjini Moshi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 23 June 2017

demo-image

Matukio : Kijiji cha Shujaaz Chafunguliwa katika Mashindano ya EAC 2017 Mjini Moshi






_MG_0865

_MG_0872

Mwakilishi wa Taasisi ya Wel tel Story ,watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz,Allan Lucky akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu kufunguliwa kwa kijiji cha Shujaaz katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki maarufu kama East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika shule ya Sekondari Moshi Ufundi .

_MG_0827

Baadhi ya Wageni wakijiandikisha kabla ya kuingia katika kijiji hicho ambako kumekuwa kukitolewa mafunzo mbalimbali hasa ya Kilimo .

_MG_0832

Mratibu wa Tafiti wa Mradi wa Shujaaz,Winnie Nyato akitoa tiketi kwa mmoja wa watoto waliotembelea kijiji cha Shujaaz .

_MG_0834

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma ,Mohamed Kombo anayejishughulisha na Kilimo cha matunda akizungumza na vijana waliofika katika kijiji cha Shujaaz kuona namna gani wanaweza kuhamasika na kuingia katika shghuli za Kilimo.

_MG_0848

Mjasiliamali Khalfa Muslim akitoa elimu jinsi ya kutengeneza mchanganiko wa Matunda kwa vijana waliotembelea kijiji cha Shujaaz kilichopo katka viwanja vya Shule ya sekondari Moshi Ufundi yanapofanyika mashindano ya East Africa Cup 2017.

_MG_0851

Mjasiliamali Holo Bukombe akionesha bidhaa mbalimbali ambazo amekuwa akiziweka katika vifungashio maalumu na kuongeza thamani ya bidhaa husika.

_MG_0852

Afisa Masoko wa kamuni ya YARA Ltd ,Linda Byaba akitoa elimu kuhusu kilimo bora na chenye tija na jinsi ya kuongeza thamani ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya Mbolea kwa Mwakilishi wa taasisi ya Wel tel Story ,Alan Lucky.

_MG_0858

_MG_0855

Muonekano wa kijiji cha Shujaaz kilichopo katika Shule ya Sekondari Moshi Ufundi ambako elimu mbalimbali hususani za Kilimo pamoja na michez kwa vijana imekuwa ikitolewa.

_MG_0838

_MG_0840

_MG_0837

_MG_0842

Baadhi ya watoto wakishindana michezo mbalimbali (Games) katika kijiji cha Shujaaz.

_MG_0860

Vijana wengine wamepaa fursa ya kucheza mchezo wa mitupo ndani ya kijiji hicho.

_MG_0861

Vijana wengine walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hasa vya kuimba na kucheza na kuambulia zawadi kutoka Shujaaz.




Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *