Fasheni : Maonesho ya Swahili Fashion Week Yafana Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 5 June 2017

Fasheni : Maonesho ya Swahili Fashion Week Yafana Jijini Dar es Salaam



Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Roberto Mengoni (kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunifu wa Mavazi nguli Mustafa Hassanal pia Mwasisi na Mtendaji Mkuu wa Basila Mwanukuzi Foundation, Basila Mwanukuzi katika maonesho ya Mavazi na bidhaa za Kitamaduni nyumbani kwa Balozi huyo Kando ya Barabara ya Kenyatta Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Maonesho hayo yaliratibiwa na Swahili Fashion Week. (Picha zote na Robert Okanda Blogspot)

Mbunifu wa Mavazi nguli Mustafa Hassanal akiwa pamoja na Mbunifu mavazi Mkongwe Ailinda Sawe (kulia) na Mbunifu mchanga, Binti wa Ailinda walipokutana katika maonesho hayo.

Mbunifu wa mavazi, Maryimaqulate Kavishe (kulia) akiwahudumia wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo.

Mbunifu wa mavazi, Jesca Matei (kushoto) akiwasikiliza wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo.

Mshiriki wa maonesho hayo Coleta Mzena (kushoto) akitabasamu kwa kamera pamoja na wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo.

William Gilhi akiwaonesha wageni bidhaa za Kampuni ya African Splash zinazopatikana pia online walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho hayo.

Kazi za michoro pia zilikuwepo katika maonesho hayo.



Wageni bidhaa wakichagua bidhaa zizizowavutia walipotembelea moja ya mabanda katika maonesho hayo.

Hapo upo saafi' Mbunifu wa Agretifela, Agnes Felician akimhamasisha mteja wake kununua moja ya bidhaa katika banda lake.

Wabunifu wa Giftedhand, wakiwa katika banda lao.

Wageni wakijionea bidhaa walipotembelea mojawapo ya mabanda katika maonesho hayo.





Mbunifu nguli Jamila Vera Swai naye akiandaa bidhaa zake kwa wageni waliojitokeza katika maonesho hayo.

Mbunifu wa Mavazi nguli Mustafa Hassanal akiwa katika kumbukumbu na Mwasisi na Mtendaji Mkuu wa Basila Mwanukuzi Foundation, Basila Mwanukuzi katika maonesho ya Mavazi na bidhaa za Kitamaduni nyumbani kwa Balozi wa Italia Kando ya Barabara ya Kenyatta Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Maonesho hayo yaliratibiwa na Swahili Fashion Week.

Mbunifu wa Mavazi pia Mtendaji Mkuu wa Kasikana Collection, Bertha Komba (kushoto) akiwa na Modal Bint Sadiq katika maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment