Michezo : Serengeti (U17 ) Yaibamiza Burundi kwa bao 3 -0 , - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


31 Mar 2017

Michezo : Serengeti (U17 ) Yaibamiza Burundi kwa bao 3 -0 ,




Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba imeanza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki kwa kichapo cha bao 3-0 na Timu ya Vijana maarufu kwa jina la Serengeti Boys.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 20 na Muhsin Malima Makame bao la pili lilifungwa dakika ya 38 na Nickson Clement Kibabage huku bao la tatu likifungwa kwa mkwaju wa penati na kepteni Kevin Nashon Naftal dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.

Mchezo wa marudiano wa timu hizi utachezwa Jumamosi hapa hapa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Kikosi cha Burundi chini ya Miaka 17 kilichoanza dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania. Picha na habari/ Faustine Ruta.

Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa KaitabaViongozi mbalimbali walikuwepo


Mgeni rasmi akisalimiana na Wachezaji wa Serengeti Boys

Mgeni Rasmi na viongozi wengine wakisalimiana na Viongozi na wachezaji wa akiba wa Burundi

Nyimbo za mataifa yote mawili ziliimbwa kabla ya mechi kuanza

Taswira kabla ya mtanange

Viongozi wa Timu ya Serengeti Boys

Serengeti Boys wakipasha kabla ya Mtanange

Picha ya pamoja manahodha na waamuzi













Kipindi cha pili kilimalizika Serengeti Boys wakiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Timu ya Burundi. Picha na habari/ Faustine Ruta.Wanaangalia Mubashara bila Kiingilio!!!

Mchezaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola wa Serengeti akiendesha mpira kipindi cha pili
Oscar Mkomola(katikati) wa Timu ya Serengeti akiwekwa kati
Kim na Bakary Shime wakiteta huku mtanange ukionekana kuwa mtelezo kwao kipindi cha pili katika mchezo wa karafiki leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba. Kocha Bakar Shime ataiongoza tena Serengeti Boys siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa pili.


Kipa hakuona kitu!

Nahodha wa Serengeti Boys Kevin Nashon Naftali dakika ya 72 ndiye aliyewafungia bao hilo baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.

Mchezaji wa Serengeti Boys (kushoto) akipeta kwa bao lao la tatu

Bao tatu 3-0

Serengeti wakifurahia moja ya bao la mkwaju wa penati


Shangwe! 3-0


Chupuchupu afunge bao lingine!

Assad Ally Juma wa Serengeti Boys(kushoto) akiufukuzia mpira

Clement Kibabane akimiliki mpira kipindi cha pili mwishoni

Kibabane tena na mpira

Mchezaji wa Serengeti Boys (kulia) Ibrahim Abdallah Ally akimnyatia mchezaji wa Burundi

Burundi wakiwa hoi baada ya kuzidiwa ujanja

Dakika 90 zilikamilika hivi....

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad