Matukio : DC Korogwe Aonya Matumizi mabaya ya Fedha za Miradi ya Maendeleo - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Feb 2017

Matukio : DC Korogwe Aonya Matumizi mabaya ya Fedha za Miradi ya Maendeleo





Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha Azidu Kaonekana wa pili kulia ambao wameshirikiana na A Better World kutoka Canada kufanya ujenzi wa majengo matatu ya maabara kwenye shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayan

Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Martha Kusare kulia akipokea msaada wa sola ya mobisol kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema ili kuweza kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi yao ambapo sola hiyo na ujenzi wa maabara tatu zilizojengwa na taasisi hiyo iligharimu kiasi cha sh.milioni 75

Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka akifuatilia maendeleo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wilayani korogwe Mkoani Tanga

Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka kulia akiteta jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Patema Jerome Massawe wakati wakitembelea maabara hiyo

Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka wa pili kulia akiangalia namna wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wanayofundishwa masomo ya sayansi mara baada ya kukamilika maabara hiyo

Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka kulia akiteta jambo na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Patema,Jerome Massawe



Muonekano wa Majengo ya maabara hizo











WATUMISHI katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wameonywa kuacha kutumia vibaya fedha za miradi zinazotokana na wafadhili kwenye maeneo yao kwani watakaobainika kufanya hivyo watashughulikiwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel wakati akipokea taarifa ya umalizaji wa majengo ya matatu ya maabara yalijengwa na taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayani humo.

Aidha wao kama viongozi wa serikali wilayani humo hawatakuwa na mdhara na watumishi ambao watabainika kuihujumu miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao na wafadhili mbalimbali kwani kufanya hivyo kunachangia kurudisha nyuma kasi ya ukuaji wa maendeleo.

“Nisema wazi kuwa watumishi badilikeni kwani mimi kama kiongozi wa wilaya hii sitamfumbia macho mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo cha maendeleo kwenye wilaya hii na niwaonye wenye tabia kama hiyo waiache mara moja.

Aidha alisema lazima watu wabadilike hasa wale wanaopewa majukumu ya kusimamia miradi hiyo kutoka kwa wafadhili na wawe wawazi wakati wa utekelezaji wake ili kujenga heshima kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

“Baadhi yetu tunatumia fursa hizo vibaya na kujinufaisha kupitia fedha za wafadhili kinyume na hitaji husika,kufanya hivyo kunaweza kuwakimbiza wadau hao wa maendeleo na kutia doa kwa Taifa”Alisema Gabriel.

Awali akizungumza katika kikao hicho Afisa Elimu sekondari Halmashauri ya Korogwe Vijijini Patricia Mbigili alisema pamoja na jitihada kubwa ambazo wanazifanya kuhakikisha wanakamilisha suala la maabara lakini mpaka sasa zilizokamilika ni 5 kati ya 78 katika shule 26,ambapo kunahitajika maabara 3 kwa kila shule ikiwa ni za chemia,physician na bioligia.

Alisema ili kukabiliana na tatizo la ufaulu wa masomo ya sayansi
katika shule za sekondari maabara na uwepo wa walimu wa masomo hayo unahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kuwajengea uwezo wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

Mbigili alisema jukumu la kuboresha miundombinu ya shule na makazi ya walimu ni la wananchi wote,serkali na taasisi zinazojitolea ili kutimiza azma ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu kama ilivyoanza kwa madawati na elimu bure.

Naye kwa upende wake, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Azidu Kaoneka alisema umaliziaji wa maabara 3,nyumba 1 ya walimu na kuwawekea kifaa cha kuzalisha umemekupitia jua (mobisol) ambapo kiasi cha shilingi milioni 75 zimetumika.

Azidu alisema taasisi hiyo inaimani kubwa kwa kushirikiana na wananchi pamoja na serikali wanaweza kujenga mazingira rafiki ya walimu na wanafunzi kwa kuboresha miundombinu ya mashule pamoja na nyumba za walimu kama ilivyofanyika shuleni hapo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad