Kifo : Wengi Wajitokeza Kumuaga Blogger na Mwanachama wa TBN, Jennifer Livigha( Chinga One ) katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


22 Feb 2017

Kifo : Wengi Wajitokeza Kumuaga Blogger na Mwanachama wa TBN, Jennifer Livigha( Chinga One ) katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam



Pichani ni Mpendwa wetu Jennifer Livigha maarufu aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la CHINGA ONE na Mwanachama mwanzilishi wa Tanzania Bloggers Network (TBN) enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake Kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiriki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.

Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer


Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama

Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu

Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer











Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakiwa wanaaga mwili wa aliyekuwa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer 'Chinga One'







Baadhi ya ndugu wa karibu, Jamaa na Marafiki wakiwa wanaaga Mwili wa Marehemu Jennifer

Baadhi ya waombolezaji wakiwa wanaimba nyimbo za maombolezo
Baadhi ya wanachama wa TBN , ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu Jennifer katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi

Baadhi ya wanafunzi wakilia kwa uchungu


Baadhi ya ndugu, jamaa na mafafiki pamoja na wanachama wa TBN wakiwa wanawaaga wanaosafiri na mwili kuelekea Nachingwea

Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (Aliyevaa T-Shirt ya Mistari) akiongea jambo kabla ya safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi.

Baadhi ya wana TBN wakiwa katika Msiba wa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer

Safari ya kuelekea Nachingwea ikiwa imeanza ..
Picha zote na Fredy Njeje wa TBN

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad